Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

2 6 0 /

K U T A F S I R I B I B L I A

Tamathali za Semi (muendelezo)

Waniinua juu hata upeponi, na kunipandisha juu yake; nawe waniyeyusha katika dhoruba. Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni, niifikie nyumba waliyoandaliwa wenye uhai wote. ~ Ayubu 30:16-23

Bila shaka tunapata maana nzuri ya kukata tamaa kwake kutoka katika lugha hii yenye kuelezeka, lakini inayoweza kuonyesha mambo zaidi ya vile yalivyo. Mtume Yohana katika Agano Jipya anatumia lugha ya chuku katika kauli hii: “Pia kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyo andikwa” (Yohana 21:25). Kama tunatazama umilele wa Yesu Kristo, labda kauli hii ingechukuliwa kama ilivyo. Lakini kama tunaishia kwenye matendo ya Bwana Yesu katika ubinadamu wake (ambao naamini ndicho Yohana anachomaanisha) basi hii hakika ni matumizi ya chuku. Inaonyesha vitu visivyo na uzima kana kwamba vina uzima na utu, kawaida inajionyesha sana mtu anapotumia lugha ya dhahania na hisia. Biblia inasema katika kitabu cha Hesabu 16:32,». . . Nchi ikafunua kinywa chake na kuwameza . . .»Ikimuongelea Kora na watu wake. Hapa nchi inapewa nafsi kana kwamba ina mdomo wa kuwararua watu hawa. Bwana Yesu anatumia tashihisi katika maneno haya, “Ee Yerusalemu, Yerusalemu uwauwaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku avikusanyavyo pamoja vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!” (Mt. 23:37). Mji wa Yerusalemu hapa unapewa uhai. Lengo la Bwana lilikuwa kwa ajili ya watu wa mji ule, lakini bado alichagua kuuongelea mji kana kwamba ndio watu wale. Tena, Bwana wetu anaipa uhai kesho katika maneno haya: “basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.” (Mt. 6:34). Hapa kesho imeelezwa na sifa za nafsi ya kibnadamu, kana kwamba imezingirwa na hofu nyingi. Tashihisi

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker