Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 2 6 1

K U T A F S I R I B I B L I A

Tamathali za Semi (muendelezo)

Ritifaa

Hii ni ajabu lakini ni mfano wa picha ambao unaonyesha zaidi kana kwamba mzungumzaji alikuwa anazungumza mwenyewe katika hali fulani ya kujiongelesha. Kwa mfano, Daudi anasema kwa mwanaye aliyekufa, “Ee mwanangu Absalomu, mwanangu! mwanangu Absalomu! Laiti ningelikufa badala yako, Absalomu mwanangu, mwanangu!” (2 Sam. 18:33). Ni aina gani ya uchungu aliokuwa nao Daudi; hakuna namna nyingine ya hisia ambayo inaweza kuonyeshwa zaidi ya hii. Kisha kuna matumizi ya mfano huu ambao wafalme wa dunia wanatumia kuonyesha mji ulioanguka, “Ole! ole! Mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.” (Ufu. 18:10). Tamathali hii ya semi inaonekana inatumika hasa kuonyesha hisia za ndani. Vivyo hivyo, inakamata hisia zetu kwa urahisi na kututengenezea shauku. Hii ni moja ya tamathali ya semi ambayo wengi wetu hatujawahi kuisikia, lakini huwa tunaitumia katika mazungumzo yetu ya kila siku. Tunasema,“hii ndio saa yake” huku hatumaanishi kwamba ni saa yenye dakika sitini. Tuna maanisha huu ni muda wa utukufu, au wa mateso, au chochote ambacho tunahusiana nacho katika hali yake ya sasa. Tumetumia sehemu ndogo kumaanisha kitu kizima. Katika Maandiko inatokea katika kifungu cha maandiko kama hiki: Katika Waamuzi 12:7 tunaambiwa Yeftha alizikwa “katika miji ya Gileadi” (Kiebrania) ingawa kimsingi ni mji mmoja tu ndio unaozungumziwa; katika Luka 2:1 “ulimwengu wote” Imetumika kuonyesha ulimwengu wa Dola ya Kirumi; katika Kumbukumbu la Torati 32:41 “Nikiunoa upanga wangu wa umeme, Mkono wangu ukishika hukumu, nitawatoza kisasi adui zangu, nitawalipa wanaonichukia”. Labda mpaka sasa tumeona vya kutosha thamani na kuenea kwa hizi tamathali za semi kunavyotusaidia kutambua uhalisia na umuhimu ambo zinaongeza katika lugha ya Biblia. Pia, katika kutafsiri, uhakiki wetu unatakiwa kuondoa utata uliopo katika aina hizi, katika kujifunza kwetu Biblia. Taniaba

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker