Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 2 7 3
K U T A F S I R I B I B L I A
Utilisation d’outils de référence pour interpréter la Bible (suite)
Vitabu vya Miongozo ya Biblia, Biblia ya Kujifunzia na Vitabu vya Mafafanuzi Kutoa wazo la kitaalamu kuhusiana na historia, muktadha na maana ya andiko. Kuelewa Mazingira ya Asili na kutafuta Kanuni za Kibiblia.
Zana Saidizi za Kileksimu, Tafsiri za Mistari za Neno kwa Neno, na Uchanganuzi wa maneno Kutoa taarifa juu ya maana, matumizi, na sarufi ya maneno ya Biblia na lugha yake.
Biblia za Mada, Vitabu vya kufundishia, na Masomo kutokana na Jumbe maalum Kutoa muhtasari wenye kueleweka sana wa vifungu vya maandiko kuhusiana na mada iliyotolewa.
Kusudi
Hatua ambayo Kuna Faida Zaidi
Kuelewa Mazingira ya Asili na Kutafuta Kanuni za Kibiblia.
Kutafuta Kanuni za Kibiblia
1. Baada ya kuwa umefanya uchunguzi wako, na umefanya maamuzi ya mwanzo kama unavyoamini kwamba hicho ndicho kifungu cha Biblia kinafundisha, kipe kifungu hicho mada ya kibiblia au kitheolojia. 2. Kwa kutumia mada hiyo, angalia katika zana za marejeo ya mada kuchunguza maandishi mengine yanayohusiana na jambo hilohilo moja, na husianisha maana zao katika kujifunza kwako. 3. Usiogope kuboresha ugunduzi wako kama kuna taarifa mpya ambayo inaongeza mwanga katika kile unachojifunza. Uwasilishwaji wa kina na wenye tija kuhusu mada mbalimbali, jumbe na dhana za kitheolojia zilizoongelewa katika kifungu cha Maandiko. Usifanye orodha ndefu ya mada toka kwenye vifungu husika kuwa MBADALA wa kuchunguza kwa kina andiko moja moja na kifungu cha Maandiko ili kupata kweli inayofundishwa.
1. Chagua maneno au kauli katika kifungu cha Maandiko ambazo zinatumika kama maneno ya msingi ya kuyafafanua ili kuelewa maana ya jumla ya kifungu hicho cha Maandiko. 2. Kwa kutumia konkodansi, leksimu au zana nyingine za kiisimu, tazama maana mbalimbali za neno hilo katika muktadha wa kitabu, mwandishi, wale waliokuwa karibu naye, Biblia na hatimaye wakati wa kuandikwa. 3. Ruhusu maana mbalimbali za kibiblia kuonyesha tofauti ya madai yaliyo katika somo lako juu ya nini kifungu cha Maandiko kilimaanisha kwa wasilikizaji wa asili na nini kinamaanisha leo. Maarifa mengi ya kitaalamu yameotolewa katika kila hatua ya kutengeneza, kutumia, na kutoa maana ya lugha za Biblia katika muktadha wake wa kihistoria na kidini. Usijifanye kana kwamba maarifa ya maana za asili YANABATILISHA maarifa muhimu ya andiko katika lugha yako.
1. Baada ya kuwa umekamilisha utafiti
wako wa awali, chagua kitabu kimoja au viwili vya mafafanuzi na upime kama vinaendana na yale uliyoyagundua katika
Hatua za kufuata
kujifunza kwako. 2. Chunguza yale
uliyoyagundua dhidi ya yale ambayo waandishi 2 mpaka 3 wameyaandika kuona kama maarifa yako yanaendana na maana walizozitoa wao.
Mawazo bora ya kitaalamu juu ya historia na maana za maandiko mbalimbali katika Biblia.
Faida
Fanya utafiti na tafakari yako mwenyewe kabla ya KUTEGEMEA mawazo ya mtafsiri wako unayempenda Zaidi.
Tahadhari ya Msingi
Kutegemeka
Nzuri
Nzuri
Bora
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker