Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
2 7 8 /
K U T A F S I R I B I B L I A
K I A M B A T I S H O C H A 2 9 Namna ya Kutafsiri Simulizi (Hadithi) Mch. Dkt Don L. Davis
Hadithi zote zina umbo maalum na zinakuwa na vipendele kadhaa ambavyo vinafanya iwezekane kupata ukweli wa hadithi, ambao unaweza kuwa wa kihistoria au wa kufikirika, katika namna ambayo ina nguvu, inatia changamoto na kuburudisha.
Vipengele katika Kujifunza juu ya Simulizi (Hadithi)
I. Zingatia kwa umakini mkubwa MUKTADHA wa hadithi.
A. Eneo: Sehemu gani kijiografia hadithi hiyo inatokea?
B. Mazingira yanayoizunguka: Ni taarifa gani kimazingira zinaihusu hadithi?
C. Mpangilio wa muda (wakati): Ni vipengele gani vya muda vimo katika hadithi?
D. Mazingira ya kiutamaduni na kihistoria yanayoizunguka hadithi: Ni taarifa gani zilizopo za kiutamaduni na kihistoria katika hadithi?
II. Watambue WAHUSIKA wa hadithi.
A. Ni akina nani wahusika wakuu wa hadithi? “shujaa” na “adui”?
B. Zingatia mfumo halisi na taarifa za vitendo, mazungumzo, na matukio ya wahusika
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker