Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
2 8 6 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Funguo kwa Utafsiri wa Biblia (muendelezo)
7. Tafuta kuelezea: • Vifungu ambavyo havieleweki kwa kauli zinazoleta maana zaidi. • Sehemu zenye mifano kulingana na mafundisho yaliyomo katika Maandiko. • Agano la Kale kwa kutumia Agano Jipya.
8. Z ingatia muktadha wote wa kitabu na vifungu vya Maandiko ambamo andiko lolote husika linapatikana.
9. M tambue mwandishi wa kibinadamu na hadhira iliyokusudiwa. Anza kwa kujaribu kugundua nini mwandishi alikuwa anajaribu kusema kwa hadhira yake ya kwanza. “kifungu cha Maandiko hakiwezi kumaanisha kile ambacho hakijawahi kumaanisha.”
Kuelewa Hali ya Mazingira ya Asili
10. T umia taarifa kuhusu maandishi ya kale, lugha, sarufi, muundo wa fasihi, na utamaduni ili kugundua maana iliyokusudiwa na mwandishi.
11. Z ingatia sana tanzu na vyanzo vya lugha zilizotumiwa na mwandishi, kisha tafsiri Maandiko kwa usahihi, hili linamaanisha tunachukua maana ya wazi za lugha kama ambavyo huwa inatumika katika tanzu hiyo.
12. T afuta mawazo, maadili na kweli ambazo hadithi inaamuru, au unabii unajaribu kuwasilisha. Tafuta kueleza kanuni hizo katika njia ambayo ni kweli na ina manufaa kwa watu wote, kwa wakati wote na hali zote.
Kutafuta Kanuni za Jumla
13. T umia andiko kutafsiri andiko. Ili kuelewa kila sehemu binafsi ya andiko, linganisha sehemu hiyo ya Maandiko na ujumbe wa Biblia nzima. Baada ya kuwa uelewa huu umefikiwa, mtu inabidi atafsiri upya uelewa wake wa andiko zima (theolojia na fundisho) kulingana na ufahamu wa taarifa mpya
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker