Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 2 8 7

K U T A F S I R I B I B L I A

Funguo kwa Utafsiri wa Biblia (muendelezo)

uliopatikana kutoka kwenye kifungu hicho cha Maandiko (Mzunguko wa kihemenetiki).

14. E lewa kwamba sababu za kuandikwa, mila, na masuala ya maisha, ni mambo muhimu katika mchakato wa kutafsiri Maandiko. Kanuni lazima zieleweke, ziwe na mantiki na zenye utetezi; na ziendane na namna ambavyo wakristo wametafsiri Maandiko katika kipindi chote cha historia; na lazima zisaidie kuyafanya maisha ya mwanadamu yalete maana.

15. K wa umakini mkubwa ondoka kutoka kwenye kile ambacho Maandiko “yalimaanisha” Kwenye hadhira ile ya asili mpaka kile “yanachomaanisha” Kwa msomaji wa sasa.

Kutumia Kanuni za Jumla kwa ajili ya Sasa

16. T umia kweli za ujumla kwa hali mahususi ambazo watu wanakabiliana nazo leo. • Kumbuka kwamba Roho Mtakatifu ndiye kiongozi wa kwanza katika kuitendea kazi kweli. Muulize yeye kwa ajili ya uongozi wake kuhusu maana kwa ajili ya matumizi ya siku za leo na katika maombi tafakari kuhusu maana ya andiko. • Tafuta uongozi wa Roho Mtakatifu kwa kuangalia namna alivyowaongoza Wakristo wengine(kutoka ndani na nje ya dhehebu lako) kutafsiri maana na matumizi ya Maandiko kwa leo.

17. W eka kanuni na utendaji wake katika lugha ambayo inaleta maana kwa wasomaji wa sasa.

18. W eka mtazamo wako kwenye “malengo muhimu ya mwisho”. Lengo la kujifunza Biblia ni kumfanya msomaji akue katika maisha na upendo kwa Yesu Kristo, kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Sio maarifa peke yake bali kubadilishwa maisha ndio lengo haswa la kutafsiri Biblia.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker