Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 3 7

K U T A F S I R I B I B L I A

2. Kwa sababu maandiko yamevuviwa na Mungu, tunasisitiza zaidi kwamba maandiko pekee ndio mamlaka ya mwisho na kamili kwa mambo yote yahusuyo Kanisa, katika kile tunachoamini na kile tunachofanya (fundisho la kutoweza kukosea ).

II. Nadharia za Uvuvio: Je, Roho Mtakatifu aliwaongoza kwa kiasi gani waandishi wa kibinadamu? Nadharia hizi zinajaribu kujibu swali la jinsi Bwana, Roho, alivyowavuvia waandishi ili matokeo ya uandishi wao yaitwe “yaliyoongozwa na Mungu.”

Muundo wa hoja katika sehemu hii umechukuliwa kutoka kwa H. Wayne House, “Theories Of Inspiration.” Charts of christian theology . Grand rapids: Zondervan, 1992.

1

A. Nadharia ya Kiimla: uandishi wa kibinadamu usioathiriwa na akili, tabia na hali za kibinadamu.

1. Mwandishi wa kibinadamu alikuwa chombo tu cha kazi katika mikono ya Mungu.

2. Mwandishi aliandika kila neno kama Mungu alivyolitamka (kunakili neno kwa neno, kama karani).

3. Mfumo huu wa imla unalinda maandiko dhidi ya makosa ya kibinadamu.

4. Majibu kuhusu Nadharia ya Kiimla

a. Hili haliwezi kuwa kweli kwa sababu vitabu vya Biblia vinaonyesha tofauti nyingi sana za uandishi, lugha, na usemi.

b. Kwa nini basi Mungu hakutupa tu kitabu kizima?

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker