Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
3 8 /
K U T A F S I R I B I B L I A
B. Nadharia ya hisia (intuition) au uvuvio wa asili : uandishi wa wanadamu wenye vipawa na ufahamu wa kiwango cha juu.
1. Roho Mtakatifu alichagua watu wenye vipawa vya hekima ya kina ya kiroho kuandika Biblia.
2. Waandishi waliandika Biblia kutokana na uzoefu wao wenyewe na ufahamu wao.
1
3. Majibu kuhusu Nadharia ya hisia (intuition) au uvuvio wa asili : Biblia yenyewe inasema kwamba Mungu, Roho, ndiye mwandishi wa maandiko, sio wanadamu aliyechaguliwa au mwenye karama za pekee, 2 Pet. 1:20-21.
C. Nadharia ya kuangaziwa : uandishi wa kibinadamu ulioongezewa uwezo.
1. Roho Mtakatifu alikuza uwezo wa kawaida wa waandishi wa kibinadamu.
2. Uwezo huu ulioimarishwa uliwawezesha waandishi kupokea na kudhihirisha mafunuo maalum yahusuyo kweli za kiroho.
3. Majibu kuhusu Nadharia ya kuangaziwa : maandiko hayazungumzii tu waandishi wa kibinadamu ambao waliandika kwa karama za ziada, lakini yanazungumzia pia wale walionena maneno yenyewe ya Mungu (“Bwana asema,” ling. na Rum. 3:2).
D. Nadharia ya Viwango vya Uvuvio : uandishi wa kibinadamu wenye viwango tofauti (vikubwa na vidogo) vya uvuvio.
1. Sehemu fulani za maandiko zimevuviwa zaidi kuliko zingine.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker