Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 3 9
K U T A F S I R I B I B L I A
2. Sehemu zinazohusika na mafundisho muhimu au ukweli wa kimaadili zimevuviwa zaidi kuliko zile zinazohusu historia, uchumi, utamaduni, n.k.
3. Baadhi ya sehemu za Biblia zinaweza kuwa hazikuvuviwa hata kidogo.
4. Majibu kuhusu Dhana ya viwango vya uvuvio:
1
a. Maandiko yote yamevuviwa na Mungu, 2 Tim. 3:16-17.
b. Kuamini juu ya viwango tofauti vya uvuvio hakuna mantiki yoyote ukizingatia mafundisho ya Yesu kuhusu Neno la Mungu, Mt. 5:17-18; Yoh. 3:34-35; 10:35.
c. Ni nani anayetuambia ni sehemu zipi zimevuviwa zaidi au kidogo?
E. Nadharia ya Uvuvio Kamili (Maneno yote) : uandishi wa kibinadamu usioathiri Kusudi la Mungu.
1. Maandiko yanaonyesha mambo ya kimungu na ya kibinadamu katika uandishi wake.
2. Nakala nzima ya maandiko, ikijumuisha uchaguzi wa maneno ambayo mwandishi alichagua, ni matokeo ya utendaji wa Mungu.
a. Yamewasilishwa kwa kuzingatia vigezo na masharti ya kibinadamu .
b. Yamewasilishwa katika lugha na nahau za kibinadamu.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker