Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

5 6 /

K U T A F S I R I B I B L I A

uvuvio wa maandiko, umuhimu wa andiko kufasiri andiko, na dhana ya ufunuo endelevu ambao unafikia kilele katika ufunuo wa Kristo. Mbinu ya Hatua Tatu ya ufasiri wa kibiblia inalenga kuziba pengo lililopo kati ya ulimwengu wa maandiko na ulimwengu wetu wa sasa, kuelewa muktadha na mazingira ya asili, kugundua kanuni za Biblia, na kuweka uhusiano kati maandiko na maisha ya kila siku. Ili kutafsiri Neno la Mungu ipasavyo, ni lazima tuandae mioyo yetu, akili zetu, na nia zetu kulisoma kwa unyenyekevu na kwa uthabiti, kulichanganua kwa uangalifu, na kulitii kwa moyo wote, yote kwa utukufu wa Mungu. Maandiko yamevuviwa kupitia nguvu na utendaji wa Roho Mtakatifu. Suala la uandishi wa mwanadamu na msukumo wa kimungu limefafanuliwa kupitia nadharia kuu tano, Hizi zinahusisha Nadharia ya Uvuvio wa Kiimla , Nadharia ya Uvuvio wa kihisia au uwezo wa usili , Nadharia ya Kuangaziwa, Nadharia ya uvuvio wa sehemu, na Nadharia ya Uvuvio wa neno kwa neno au Uvuvio Kamili. Nadharia ya Uvuvio wa neno kwa neno au Uvuvio Kamili ni imani ya kwamba maandiko yote ya Biblia, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa maneno aliyoyachagua mwandishi, ni matokeo ya uongozi na uchaguzi wa Mungu. Uhakiki wa kisasa wa Biblia unajaribu kufuatilia asili ya maandiko kwa kuanzia na matukio ya awali yanayonenwa katika Biblia hadi simulizi halisi za matukio hayo yaliyorekodiwa katika vitabu vya kikanoni vya maandiko. Uhakiki huu unalenga kufuatilia ujumbe wa Mungu tangu tukio halisi lililorekodiwa na muktadha wake hadi tafsiri ya maandiko tuliyo nayo leo. Vipengele muhimu vya uhakiki wa kisasa wa Biblia vinahusisha uhakiki wa muundo (kufuatilia mapokeo simulizi), uhakiki wa chanzo (kutafuta vyanzo vya maandiko), uhakiki wa lugha (lugha, maneno, na sarufi), uhakiki wa maandishi (nakala za maandishi), uhakiki wa kifasihi (kanuni za fasihi), uhakiki wa kikanoni (jinsi vitabu vilivyochaguliwa), uhakiki wa uandishi (madhumuni ya waandishi), uhakiki wa kihistoria (historia na utamaduni), na uhakiki wa tafsiri. Licha ya madai yanayotolewa na wasomi wengi leo, tunaweza kuwa na uhakika kwamba maandiko kwa kweli ni Neno la Mungu linaloishi na kudumu milele. Ikiwa ungependa kujifunza kwa kina baadhi ya mawazo ya somo hili la Kuvuviwa kwa Biblia: Chimbuko na Mamlaka ya Biblia , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Bacote, Vincent, Laura C. Miguelez, and Dennis L. Okholm. Evangelicals & Scripture: Tradition, Authority and Hermeneutics . Downers Grove, IL: Intervarsity Press, 2004.

1

Nyenzo na bibliografia

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker