Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 5 7

K U T A F S I R I B I B L I A

Barton, John. People of The Book: The Authority of The Bible In Christianity . Louisville, KY: Westminster John Knox Press, 1989. Bruce, F. F. The Canon Of Scripture . Downers Grove, IL: Intervarsity Press, 1988. ------. The New Testament Documents: Are They Reliable? Grand Rapids: Eerdmans Publishing Company, 2003. Fundisho la asili na uvuvio wa maandiko linatumika moja kwa moja katika huduma yetu kwa wengine. Kukosa imani katika nguvu za Neno la Mungu kutaathiri kwa namna nyingi jinsi unavyohubiri, unayemhubiria, na kile unachotarajia kutokana na huduma yako ya Neno. Chukua muda sasa kuchunguza matokeo ya kweli hizi muhimu kuhusu maandiko yenye pumzi ya Mungu, na utafute kutumia maarifa haya katika huduma halisi na ya vitendo kwenye eneo ambalo unatumikia na kufundisha. Unapojadili na kutafakari juu ya kweli hizi katika somo hili lote, yawezekana mawazo kadha wa kadha “yameibuka” ndani yako kwa uzito na umuhimu mkubwa na unaamini yatakufaa katika maisha na huduma yako mwenyewe, na huenda ni mambo yanayohitaji muda zaidi wa maombi, kutafakari, na kujifunza wiki hii ijayo. Angalia kwa umakini mwelekeo mahususi ambao Roho Mtakatifu anataka uchukue kuhusiana mada ya mamlaka na uvuvio wa maandiko, na ujasiri unaotokona na ufahamu huu tunapokiri ahadi za Neno, kutii amri zilizomo, na kuthamini yale linayosema kuhusu Mungu, Mwana wake, na Ufalme. Moja ya mambo muhimu unayopaswa kufanya kama sehemu ya kujifunza kwako ni maombi na maombezi ya wazi wazi na yenye malengo mahususi kwa niaba ya wanafunzi wenzako darasani. Kwa kuzingatia kweli mbalimbali, changamoto na mahitaji mnayoshirikishana muda wote, tumia muda na uombe kimahususi kabisa kuhusu mahitaji na kila linalowahusu wanafunzi wenzako. Kamwe usipuuzie nguvu ya maombi yafanywayo kwa uaminifu kufanya kweli ya Mungu iwe hai katika maisha yetu. Ni pale tu Roho Mtakatifu anapotupa mafunuo na neema yake ndipo tunaweza kubadilishwa, na kuifanya kweli iwe halisi katika maisha yetu (1 Kor. 2:9-16).

Kuhusianisha Somo na Huduma

1

Ushauri na maombi

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker