Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 8 5
K U T A F S I R I B I B L I A
I. Tujifunze kupitia andiko la 1 Wakorintho 9:1-14: zingatia maelezo (Fuata uchunguzi huu kwa mpangilio ule ule unaopatikana katika “Funguo za Ufasiri” katika kiambatisho). 1 Wakorintho 9:1-14 – Je! Mimi si huru? Mimi si mtume? Mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Ninyi si kazi yangu katika Bwana? 2 Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, lakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana ninyi ndinyi muhuri ya utume wangu katika Bwana. 3 Hilo ndilo jawabu langu kwa wale wanaoniuliza. 4 Je! Hatuna uwezo wa kula na kunywa? 5 Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa? 6 Au je! Ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo wa kutokufanya kazi? 7 Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi? 8 Je! Ninanena hayo kwa kibinadamu? Au torati nayo haisemi yayo hayo? 9 Kwa maana katika torati ya Musa imeandikwa, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Je! Hapo Mungu aangalia mambo ya ng’ombe? 10 Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu; kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini, naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake. 11 Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini? 12 Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo. 13 Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? 14 Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.
Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video
2
A. Mwombe Mungu afungue macho yako uweze kuitambua kweli.
1. Roho Mtakatifu ndiye mwandishi wa maandiko, 2 Pet. 1:20-21.
2. Kama mwandishi wa maandiko anaweza kutufundisha maana yake, 1 Yohana 2:20.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker