Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

9 4 /

K U T A F S I R I B I B L I A

E. Paulo, Rabi (Mwalimu wa Sheria): kutengeneza kanuni kwa ajili ya Wakorintho:

1. Kielelezo cha kwanza cha Paulo: 1 Kor. 9:10 – Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu; kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini, naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake.

2. KielelezochapilichaPaulo:1Kor.9:13–Hamjuiyakuwawalewazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?

2

3. Kanuni ya Paulo: 1 Kor. 9:14 – Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.

F. Namna Paulo anavyotambua kanuni katika maandiko:

1. Anaanza na hoja kubwa: utetezi wa utume wake.

2. Analinganisha maandiko na maandiko: 1 Wakorintho 9:10 na Kut 29:32-33; Hesabu 18:21.

3. Anaihusianisha kanuni na maisha halisi: askari, mchungaji, mkulima, mfanyakazi wa hekalu.

4. Anaitumia katika hali yake mwenyewe: 1 Kor. 9:11-12 – Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini? 12 Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker