Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 9 5

K U T A F S I R I B I B L I A

III. Tumia Kanuni za Jumla za Maisha katika Nguvu za Roho.

Tafuta mifano inayoendana na uitumie.

A. Ufafanuzi: Kutendea kazi Neno ni kitendo cha kuelekeza moyo kwenye Kweli ya Neno la Mungu kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu .

Kuhusianisha maandiko kitheolojia ni muhimu, lakini kuhusianisha maandiko vibaya kunapotosha na ni hatari. Imeonekana mara nyingi kwamba kwa sehemu kubwa kweli ya Neno inagunduliwa kwa kuhusianisha kwa namna iliyo halali kifungu na kifungu kingine, kweli na kweli iliyopo mahala pengine ndani ya Biblia. Ukweli huo ni wito wa kufanya kazi kwa uangalifu na onyo dhidi ya tabia ya kupunguza uzito na mantiki ya andiko. Uwiano wa kibiblia ni lengo muhimu. Kwa kuanzia, ili kuweka mfumo wa msingi tutakaotumia kutafsiri maandiko, tuepukane na mbinu zote za kikundi fulani tu cha watu wenye malengo binafsi, kwa kunyofoa vifungu vyenye utata na kuvitafsiri pasipo uwiano na uhusiano na maandiko mengine. (k.m. 1 Kor. 15:29). ~ Donald A. Carson. New Bible Commentary: 21st Century Edition. (electronic ed. of the 4th ed.). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1997. kufasiri ambazo zinatoa maana zinazoeleweka na

1. Kuelekeza moyo: kutendea kazi Neno kunatokana na dhamiri ambayo imekubali na nia iliyo tayari kuipokea na kuiishi kweli ya Mungu katika Neno.

2. Kwa kuongozwa na Roho: Roho Mtakatifu, yule yule anayevuvia Neno, ndiye anayeangazia moyo na kuchochea nia ya kuitikia kweli ya Mungu.

2

B. Kutendea kazi Neno kunahitaji uwezo wa kupambanua.

1. Roho Mtakatifu anahusika katika utendaji wowote wa Kweli ya Kristo katika maisha ya Mkristo, Yohana 15:26-27.

2. Ufahamu ni zawadi ya Bwana.

a. Zaburi 119:33

b. Yohana 14:26

c. Yakobo 1:5

d. 1 Yohana 2:27

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker