Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

/ 1 6 3

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

maalum la kuhudumia mahitaji ya walemavu, wazee, waliofiwa, watoto wa mazingira hatarishi na familia zilizo katika mvutano, na kuwarekebisha wahalifu wa sheria, walevi, waraibu wa dawa za kulevya na wacheza kamari sugu. 3. Ni lazima lishuhudie “kweli kama ilivyo katika Yesu” (Efe. 4:21). Hii inahusisha kazi kadha wa kadha, wakati mwingine zilizogawanywa katika makundi matatu ambayo ni kutetea au kushindania imani (apologetics), kazi tangulizi kabla ya uinjilisti, na uinjilisti halisi. Kutoa ushuhuda kunamaanisha mawasiliano ya mdomo ya injili ya kitume na dhihirisho la wazi la uwezo wake wa kuleta maisha mapya na matumaini katika mahusiano ya kibinadamu na kijamii. 4. Linapaswa kujihusisha katika kuhakikisha kwamba haki ya Mungu inatendeka katika jamii. Kipekee, kanisa linapaswa kuwa na bidii katika kukuza na kutetea uadilifu wa maisha ya familia dhidi ya talaka rahisi, utoaji mimba, mahusiano haramu ya kimapenzi, ponografia, unyanyasaji wa wanawake na watoto, na majaribio ya kisayansi yanayofanyika juu ya maisha ya vichanga. Pia Kanisa linapaswa kutafuta njia mbadala za sera mbaya ambazo zinaongeza idadi ya watu wengi wasio na makazi, wenye elimu duni, wasio na lishe bora na wasio na ajira. Linapaswa kupigania haki za binadamu na kupambana dhidi ya ubaguzi wa binadamu. Hatimaye, linapaswa kukabiliana na utengenezaji usio wa lazima wa silaha za maangamizi makubwa na kuongezeka kwa biashara ya silaha kati ya mataifa tajiri na maskini. 5. Lina wajibu wa kuonyesha kwa vitendo maana ya kuwa jumuiya iliyopatanishwa na kukombolewa katikati ya ulimwengu uliopotea, wenye dhiki na kukata tamaa. Kanisa limetumwa ili kuonyesha uhalisia wa neema ya Mungu isiyostahiliwa kwa kuonyesha matendo ya msamaha, kugawana mali na rasilimali, kwa kuondoa chuki na mashaka, na kwa kutumia mamlaka kwa ajili ya utumishi, si kwa ajili ya kutawala na kukandamiza maisha ya watu. Kanisa linapaswa kuwa ishara na wakala wa kusudi la Mungu la kuunda utaratibu mpya ambapo amani na haki yake itatawala. ~J. A. Kirk. “Missiology.” The New Dictionary of Theology. S. B. Ferguson, mh. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 435.

3

Made with FlippingBook - Online catalogs