Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

1 6 4 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

MUUNGANIKO

Somo hili linalenga juu ya miji na majiji na jukumu lake la kimkakati katika utume. Kwa sababu ya umuhimu wa mji katika suala la uteuzi wa Mungu wa mji kama ishara ya mabadiliko na usalama, na vile vile umuhimu wake katika ulimwengu wa kisasa, lazima miji ibaki kuwa kipaumbele katika huduma zote za Kikristo na maendeleo ya Ufalme. Chukua muda wa kupitia kwa umakini kweli kuu za somo hili kupitia dhana zilizoorodheshwa hapa chini. ³ Dhana ya mji inatawala ndani ya Agano la Kale na Agano Jipya, na inatupatia muhtasari rahisi wa sifa za miji ya kale. Miji katika ulimwengu wa kale ilikuwa tofauti na vijiji kwa kuwa ilikuwa ni mkusanyiko wa nyumba na majengo yaliyozungukwa na kuta, ilikuwa muhimu na yenye kuvutia kwa wakati wao, na baadhi ya miji ilitegemea miji mingine kwa ajili ya ulinzi na mahitaji muhimu. Ukweli wa kawaida katika ulimwengu wa kale, miji ya zamani ilikuwa midogo, kwa kawaida isiyo na lami, iliyoimarishwa kwa kuta nene na minara mirefu, na vituo vya serikali na mamlaka. ³ Kuhusu maana yake ya kiroho kama ilivyoainishwa katika Maandiko, miji ilihusishwa na uasi wa kibinadamu na ibada ya sanamu (k.m., Henoko, jiji la Kaini), na uhuru na kiburi (kama ilivyokuwa kwenye Mnara wa Babeli), na uovu na kutomcha Mungu (kama vile Babeli). Miji ilihukumiwa na Mungu kwa sababu ya dhambi yake (k.m., Sodoma na Gomora, Yeriko, Ninawi), na kushutumiwa kwa kujidhania kwa uongo kwamba ina usalama na uwezo (hasa, Yerusalemu). ³ Ingawa Maandiko yanahusianisha mji wa Yerusalemu na uasi wa wanadamu, yanafundisha pia kwamba Mungu aliukubali mji huo kuwa ishara ya makao yake na baraka zake. Licha ya ukweli kwamba Daudi aliushinda mji huo kwa njia ya vita, Mungu aliuchagua Yerusalemu kwa ajili yake mwenyewe, na akaamua kuufanya kuwa wenye sifa duniani. Ajabu ya Kimungu ni hii hapa: Mungu anabadilisha taswira ya kidunia ya “kujitegemea na uasi” kuwa taswira ya “ kimbilio ” (k.m. miji ya makimbilio), na picha ya upatanisho , mahali pa kuujua na kuupata msamaha na baraka zake (k.m. Yona na kisa cha Ninawi). ³ Kwa sababu ya rehema na neema ya Mwenyezi Mungu katika Kristo, tumaini lipo kwa mji wowote unaotubu mbele ya hukumu yake, unaojinyenyekeza chini ya matakwa yake, na kutafuta rehema zake mbele ya adhabu yake. ³ Kuna sababu tatu muhimu zinazo thibitisha vya kutosha kwa nini utume wa mijini lazima uwe kipaumbele cha shughuli zote za utume leo: mji ni makao ya ushawishi, nguvu, na shughuli za kiroho duniani, unazidi kuwa

Muhtasari wa Dhana Muhimu

3

Made with FlippingBook - Online catalogs