Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

1 9 8 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

A. Watu wa Mungu wanapaswa kuakisi uhusiano wa Mungu mwenyewe na maskini, wakizingatia uzoefu wao wa kihistoria katika tukio la Kutoka.

B. Mungu atadhihirisha shalom pale tutakapomfuata Bwana na amri zake.

Hitimisho

» Dhana ya umaskini inaweza kueleweka kupitia dhana ya kibiblia ya shalom , yaani ukamilifu wa jamii ya agano la Mungu. » Ijapokuwa Israeli hawakuwa waaminifu katika kuonyesha haki na uadilifu wa Mungu, msingi wa Biblia unaonyesha kwamba Mungu alijihusisha na watu maskini katika hali yao mbaya, na akawataka watu wake waonyeshe shalom hiyo katika matendo yao wenyewe kwa wenyewe kama nuru kwa mataifa. Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yametokana na video. Katika sehemu hii tumeona jinsi dhana ya umaskini inavyohusiana na dhana ya kibiblia ya shalom , au ukamilifu wa jamii ya agano la Mungu. Katika maagizo na masharti yote ya agano la Mungu, alitamani kwamba watu wake waonyeshe upendo wake wa kina na kujitolea kwa maskini. Ingawa Israeli hawakutii siku zote mapenzi yake katika kuonyesha haki na uadilifu kwa maskini, maagizo yake yalikuwa wazi. Mungu alijitambulisha pamoja na maskini katika hali yao mbaya, na aliagiza kwamba watu wake waonyeshe upendo wake kwa haki, shalom yake, katika namna wanavyotendeana wenyewe kwa wenyewe kama jamii yake ya agano. Fanya marudio ya kweli hizi muhimu, na maana yake kwa umisheni, kwa kujibu maswali hapa chini. 1. Ni nini tafsiri ya shalom , na inahusiana vipi na ufafanuzi na ufahamu wa kibiblia wa umaskini? 2. Je, ni baadhi ya vipengele gani muhimu vya kibiblia vinavyoelezea dhana ya shalom katikati ya watu wa Mungu? Kwa nini shalom haiwezi kamwe kueleweka kama matokeo ya kazi ya watu pekee, bali daima kama matokeo ya utoaji wa neema ya Mungu? Je, shalom inahusianaje na kuja kwa Masihi?

Sehemu ya 1

4

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook - Online catalogs