Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
/ 1 9 9
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
3. Eleza jinsi umaskini (na athari zake) ni kunyimwa shalom ya Mungu. Baraka, sheria, na amri za Mungu za agano zilikusudiwa jinsi gani kushinda umaskini na kuhakikisha uwepo wa haki na uadilifu kati ya watu wake? 4. Ni katika maana gani tunaweza kusema kwamba Mungu anajitambulisha pamoja na maskini katika hali zao mbaya na dhiki zao? Tukio la Kutoka linaakisi namna gani utambulisho wa Mungu na maskini na waliodhulumiwa? Israeli ilikusudiwaje na Mungu kuwa “kielelezo cha utakatifu wake, taswira ya haki na rehema zake, na nuru kwa mataifa” kupitia agano? 5. Ni zipi sababu tatu kuu za umaskini katika Maandiko, nazo zinahusianaje? Neno “maskini” katika Maandiko linaunganishwaje na dhana zingine ambazo hutumika kama visawe vyake, kwa mfano, “mjane,” “yatima,” na “mgeni?” 6. Orodhesha baadhi ya viwango vya Mungu vya kuwatendea maskini katika jamii ya agano katika Agano la Kale. Viwango hivyo vinatoaje ushuhuda, kuhusu moyo wa Mungu kwa ajili ya maskini, na vilevile hekima aliyotumia kwa watu wake ili kuondoa umaskini miongoni mwao? 7. Orodhesha viwango viwili vya agano ambavyo Mungu aliwapa watu wake na uvijadili kwa ukamilifu kulingana na maana na umuhimu wake kwa shalom . Je, viwango hivi vinawezaje kutuelekeza jinsi tunavyopaswa kuwatendea maskini leo? Toa maelezo sahihi kulingana na somo hili. 8. Katika kuangalia viwango hivi kwa jamii ya agano la Mungu, dondoo zake kuu ni zipi? Je, viwango hivi vinatoa maarifa gani kwa mitazamo yetu kuhusiana na misingi yetu ya kutenda haki, ufuasi, na umisheni leo?
4
Utume wa Kikristo na Maskini Sehemu ya 2: Kanuni na Madokezo ya Kimisheni kwa ajili ya Kufanya Huduma Mjini
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
Yesu ndiye mwanzilishi na Kichwa cha Kanisa, Jamii ya Ufalme wa Mungu ya Agano Jipya, ambayo imeitwa kuonyesha shalom ya Mungu katikati ya watu wa Mungu leo. Yesu alijitambulisha kama Masihi yule wa unabii na ahadi ya A.K. Alianzisha huduma yake ya Kimasihi kwa matendo ya kuponya walioonewa na
Muhtasari wa Sehemu ya 2
Made with FlippingBook - Online catalogs