Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

/ 2 1 1

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

III. Dondoo kwa ajili ya uelewa wa kibiblia wa utume mjini

Je, Maskini Wanawahitaji Matajiri, au Wote Wanahitajiana?

Nguvu ya Injili inadhihirishwa pale ambapo wale ambao ni ‘wenye haki’ na ‘matajiri’ wanaweza kuuelewa ujumbe wa Injili katika mkazo wake kuhusu nafasi na umuhimu wa watu maskini. Yule mtawala kijana tajiri alipogeuka kwenda zake, Yesu alisema hivi: ‘Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.... Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana’ (Mathayo 19:24-27). Mtazamo huu wa kibiblia unakabiliana na mtazamo kwamba maskini wanahitaji ukarimu wa matajiri kama wapokeaji wa kudumu wa misaada. Badala yake matajiri wanawahitaji maskini ili kujifunza kutoka kwao asili na maana ya ukombozi ambao Mungu ameleta kwa makundi yote mawili. Msingi wa kugawana mali ni wakati watu hawa waliotenganishwa kwa sababu ya mahusiano yaliyopotoka wanagundua kwamba wote wawili wanahitajiana kwa kiwango sawa. Yesu Kristo pekee ndiye anayeweza kuleta haya. ‘Mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha’ (Warumi 15:7). ~C. M. N. Sugden. “Poverty and Wealth.” The New Dictionary of Theology. S. B. Ferguson, mh. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 524.

4

A. Tangaza Habari Njema kwa maskini: iga huduma ya Yesu kwa kutangaza Habari Njema kwa maskini.

1. Waheshimu kama watu ambao wamechaguliwa na Mungu kuwa warithi wa Ufalme, Yak. 2:5.

2. Watumikie kama watu ambao Yesu amejitambulisha nao bila kujizuia: wenye njaa, wenye kiu, wageni, wagonjwa, waliofungwa, walio uchi, Mt. 25:31-46.

Made with FlippingBook - Online catalogs