Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
/ 2 1 5
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Maswali yafuatayo yaliandaliwa ili kukusaidia kufanya marudio ya maudhui ya sehemu ya pili ya video. Katika sehemu hii ya mwisho tumegundua jinsi ambavyo Yesu bila kujizuia aliungamanisha maisha yake na huduma yake kwa ukaribu sana na maskini. Akiwa Masihi na Kichwa cha Kanisa, katika huduma yake yote na kufundisha kwake alionyesha kujitoa kwake kwa wanyonge, waliopotea, na wasiojiweza wa siku zake. Inaonekana mwelekeo huu pia unahusishwa na nafasi yake kama Mtumishi Mwenye Kuteseka ambaye alitimiza unabii wa Kimasihi, yule aliyepewa utume wa kuokoa wafungwa na maskini, kutangaza Habari Njema ya Ufalme, kuanzisha jamii yake mwenyewe ya Kimasihi ambayo ingeonyesha uhai wa Ufalme huo kwa washirika wake na majirani zao. Unapopitia mambo makuu mbalimbali ya somo hili kwa kutumia maswali yaliyo hapa chini, fikiria njia ambazo Mungu anaweza kuwa anatuita sisi, kupitia maisha na huduma zetu, kuonyesha shalom ile ile ya Ufalme ambayo ilikuwa dhahiri sana katika maisha na mafundisho ya Yesu. Kama kawaida, daima uwe wazi katika majibu yako na ujibu kwa ufupi, na inapowezekana utumie Maandiko! 1. Je, uhusiano wa Yesu na Kanisa kama jamii ya ufalme mpya wa Mungu ni upi? 2. Eleza jinsi kazi ya Yesu kama Masihi ilivyozinduliwa rasmi, ilivyohakikiwa, kuthibitishwa, na kufungamanishwa katika kila njia na maskini na namna walivyopaswa kutendewa. Je, hii inatufundisha nini kuhusu kipaumbele ambacho maskini wanapaswa kuwa nacho kila wakati katika kazi ya Kanisa? 3. Inamaanisha nini kusema kwamba Kanisa ni “jamii ya ufalme wa Mungu”? Katika jukumu lake kama mwili wa Kristo, Kanisa linaitwaje kuiga na kutimiza huduma ya Kristo ulimwenguni leo? Ni kwa jinsi gani Kanisa katika kazi zake, maneno yake, na ushuhuda wake linatoa ushahidi wa maisha ya Enzi Ijayo katika ulimwengu wa leo? 4. Ni kwa maana gani tunaweza kusema kwamba kwa njia ya maisha na utume wa Kanisa, kama linavyowezeshwa na Roho Mtakatifu, shalom yenyewe ya Mungu inafurahiwa na kuonyeshwa papa hapa na sasa hivi? 5. Kwa nini ukarimu kwa wahitaji (hasa kwa wajane, yatima, na maskini) ni muhimu sana katika kazi ya Kanisa ya kushuhudia habari za Ufalme? 6. Je, ni kwa njia gani watu wa Mungu wanapaswa kuwa watetezi wa maskini na wale wasio na sauti katika jamii na maishani? Sifa za utetezi huo ni zipi, na kwa nini tunaweza kusema kwamba “kusimama mahali palipo bomoka” kwa niaba ya maskini ni alama mahususi ya utume halisi wa Kikristo?
Sehemu ya 2
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 460 4
4
Made with FlippingBook - Online catalogs