Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

2 1 6 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

7. Kwa nini maskini kamwe hawapaswi kunyanyaswa bali daima waheshimiwe na kupewa hadhi katika namna zetu zote za kushughulika nao? Ni katika maana gani ni lazima kwa wale wanaotumikia maskini wawe na uhakika kwamba Mungu anaweza kubadili hali zao, na pia kuwawezesha ili waweze kuchangia kikamilifu katika kuendeleza Ufalme wa Mungu? 8. Elezea usemi huu: “Kanisa lazima litende kwa kuzingatia kwamba Mungu amewachagua maskini.” Ni kwa maana gani tunaweza kusema kwamba Mungu amewachagua maskini kuwa matajiri katika imani (Yak. 2:5)? Kwa nini ni lazima sikuzote tuwe waangalifu hasa kuonyesha ukarimu kwa wageni na wafungwa? 9. Kwa nini kujali kwetu na huduma yetu kwa maskini lazima daima iende mbali zaidi ya kukidhi mahitaji ya kawaida na badala yake tuweze pia kutafuta kujihusisha na kubadilisha mifumo na mahusiano kwa namna ambayo itasababisha utendaji wa haki zaidi kwa niaba yao? Elezea. 10. Kwa nini kuwasaidia maskini kulingana na viwango vya Mungu vya shalom ndiyo ufafanuzi bora zaidi wa “Injili ya mafanikio”? Tunaweza kuwa na uhakika gani kwamba Mungu atafanya kwa niaba yetu ikiwa kweli tunajidhabihu kwa niaba ya maskini? Katika mafundisho ya Yesu hachukulii mali kuwa ni mbaya, bali kwamba ni hatari. Maskini mara nyingi wanaonyeshwa kuwa wenye furaha kuliko matajiri, kwa sababu ni rahisi kwao kuwa na mtazamo wa kumtegemea Mungu. Ni wao ambao alikuja kuwahubiria Injili (Luka 4:18; 7:22). Ni wao waliokuwa wa kwanza kuitwa wenye heri na kuhakikishiwa milki ya Ufalme wa Mungu (Lk. 6:20), ikiwa umaskini wao ni umaskini wa roho (Mt. 5:3). Sadaka ya maskini inaweza kuwa ya thamani kubwa zaidi kuliko ya tajiri (Mk. 12:41–44). Maskini lazima watendewe kwa ukarimu (Lk 14:12–14), na wapewe sadaka (Lk 18:22), ingawa wema ulichukuwa nafasi ya pili baada ya ibada (Yoh. 12:1–8). Kanisa la kwanza lilifanya majaribio ya kumiliki mali kwa pamoja kama jumuiya (Mdo. 2:41–42; 4:32). Kimsingi, jambao hili lilipelekea kuondolewa kwa umaskini (Mdo. 4:34-35), lakini mara nyingi limechukuliwa kwamba lilihusika katika kusababisha anguko la baadaye la kiuchumi la kanisa la Yerusalemu. Sehemu kubwa ya huduma ya Paulo ilihusika na kuchangisha fedha katika makanisa ya Mataifa ili kuwasaidia Wakristo maskini kule Yerusalemu (Rum. 15:25–29; Gal. 2:10). Makanisa haya pia yalifundishwa kuwasaidia washirika wao walio maskini (Warumi 12:13, nk.). Yakobo ni mkali hasa dhidi ya wale walioruhusu ubaguzi kwa Maskini Katika Agano Jipya

4

Made with FlippingBook - Online catalogs