Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
/ 2 1 7
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
misingi ya tofauti za mali katika jamii ya Kikristo (Yak. 2:1–7). Maskini waliitwa na Mungu na wokovu wao ulimletea utukufu (1Kor. 1:26-31). Kanisa la Laodikia lilikuwa na utajiri mwingi wa kimwili na bado lilikuwa na umaskini wa kutisha wa kiroho (Ufu. 3:17). Ufafanuzi wa kina zaidi katika Nyaraka kuhusu umaskini na utajiri unapatikana katika 2 Kor. 8-9, ambapo Paulo anaweka wazo la upendo wa Kikristo katika muktadha wa karama za Mungu na utoaji wake na hasa ule wa kumtoa Mwanawe ambaye alifanyika “maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.” Kwa kuzingatia hilo, kujihatarisha kwa umaskini wa kimwili kutaongoza kwenye baraka za kiroho, kama vile mitume walivyokuwa maskini lakini walifanya wengi kuwa matajiri (2Kor. 6:10). ~R. E. Nixon. “Poverty.” The New Bible Dictionary. D. R. W. Wood, mh. Toleo la 3 (toleo la Kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1996. uk. 945. Somo hili linaangazia uhusiano wa masikini na utume wa Kikristo. Tumechunguza dhana hii kupitia dhana ya shalom ya Mungu, iliyotajwa kwanza katika Agano la Kale kuhusiana na jamii ya agano la Mungu Israeli na namna walivyoshughulika na maskini, na kisha tukapanua mjadala wetu na kuangazia jukumu la Kanisa. Dhana zifuatazo zinaangazia mambo muhimu katika somo hili. ³ Dhana ya maskini imejengwa juu ya maono ya kibiblia ya shalom, au ukamilifu: shalom ni neno la Kiebrania linalomaanisha «ukamilifu wa jamii ya wanadamu katika ushirika na Mungu na baina yao mmoja kwa mwingine.» ³ Vipengele vya kibiblia vya shalom ni pamoja na uzima na afya njema, usalama na ulinzi, maelewano kati ya majirani, ustawi na utoshelevu wa mali, na kukosekana kwa uovu na migogoro – Amani ya kweli na kamilifu. Hili pia linajumuisha wazo la shalom kama utoaji wa Mungu kwa msingi wa neema yake, unaohusishwa na ujio wa Masihi ambaye ni Mfalme wa shalom, pamoja na shalom kama kiwango cha maisha kwa watu wa Mungu. ³ Umaskini ni kunyimwa shalom ya Mungu; baraka na upaji wake vilitolewa ili kuzuia kutokea kwa umaskini, na amri na maagizo ya Mungu kwa jamii ya agano zilikusudiwa kuhakikisha haki na uadilifu kati ya watu wa Yehova. Uaminifu kwa agano ulikusudiwa kwa ajili ya kuendeleza shalom
MUUNGANIKO
Muhtasari wa Dhana Muhimu
4
Made with FlippingBook - Online catalogs