Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

2 2 8 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Tafadhali zingatia: Ufaulu wako katika moduli hii hauwezi kupimwa na kujulikana kama hautafanya mtihani wa mwisho na kukusanya kazi zote na kuzikabidhi kwa mkufunzi wako (Fomu ya Ripoti ya Usomaji, kazi za kihuduma, kazi za ufafanuzi wa Maandiko, na mtihani wa mwisho).

Katika somo hili tulizingatia dhana ya umaskini kupitia dhana ya shalom , au ukamilifu wa jamii ya agano la Mungu. Tuliona kwamba ingawa Israeli walikosa uaminifu katika kutii wito wa agano la Mungu wa kuonyesha haki na uadilifu wake, taswira ya shalom katika agano hilo ilikuwa nzuri na ya kweli. Mungu Mwenyezi anajitambulisha na maskini katika hali yao mbaya, na anawaagiza watu wake waonyeshe shalom hiyo katika kushughulika kwao wenyewe kwa wenyewe kama nuru kwa mataifa. Kwa njia ya Yesu Kristo, haki ya Mungu ilitimizwa, na jamii mpya ikaanzishwa na Roho Mtakatifu. Kanisa, sasa limeitwa kutimiza shalom inayotarajiwa katika Agano la Kale, na Yesu ndiye mwanzilishi na kichwa cha Kanisa. Akiwa Mtumishi Mwenye Kuteseka aliyetimiza unabii wa Kimasihi wa Mungu kuhusu Masihi, sasa ameunda jamii mpya, Kanisa, ambalo utume wake ni kutangaza Habari Njema ya Ufalme kwa maskini na kujitahidi kudhihirisha maisha ya Ufalme huo kwa washirika wake na jirani zake. Maono ya utume (kama tamthilia takatifu, mapenzi ya kiungu, utimilifu wa ahadi, na kama Vita vya Milki) yanaonyeshwa wazi wazi wakati ambapo sisi, kama washirika wa Kanisa, tunapoamka na kutimiza wito wetu wa kuonyesha Ufalme wa Mungu duniani. Na, kati ya sehemu zote zinazohitaji kuonyeshwa utendaji wa Ufalme ulimwenguni leo, majiji yanahitaji kubwa la ushuhuda ulio hai kwa Kristo na Ufalme wake. Shauku yetu ya kweli ni kwamba tukubali wito huu wa kuungana na Mungu katika njama yake takatifu, katika mapenzi yake ya kiungu, kama watoto wa ahadi na wapambanaji katika jeshi la Kristo, na kufanya yote tuwezayo kuendeleza Ufalme wake hadi miisho ya dunia. Mungu wetu akujalie kuwa na mzigo kwa ajili ya walimwengu kama mtumishi wake, na kwa Roho wake Mtakatifu akuongoze katika huduma ambayo unaweza kutoa mchango wako wa kipekee wa kufanya shalom kuwa kweli katikati ya watu wa Mungu leo. Kwa utukufu wake, Amina!

Neno la Mwisho kuhusu Moduli Hii

4

Made with FlippingBook - Online catalogs