Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

/ 2 2 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

huo. Katika siku zijazo utakuwa na fursa ya kuwashirikisha wengine maarifa haya katika mazingira ya maisha halisi, mazingira halisi ya huduma. Omba kwamba Mungu akuwezeshe kutambua njia zake unapowashirikisha wengine maarifa yako kupitia kazi yako.

Katika somo hili la mwisho la moduli hii, chunguza moyo wako mbele za Bwana: je, kuna masuala yoyote yaliyosalia, watu, hali, au fursa ambazo unahitaji uongozi na mwelekeo wa Roho ili kushughulika nayo? Je, katika somo hili kulikuwa na mambo maalum kuhusu maskini na wajibu wetu kwao ambayo unahitaji usaidizi na uwezesho, mambo ya kubadilisha, kujifunza, kuacha, kuanza? Je, ni masuala gani hasa au watu gani ambao Mungu ameweka katika moyo wako ambao wanahitaji dua na maombi yako kuhusiana na somo hili? Chochote ambacho Bwana anakuambia, chukua wakati unaohitaji ili kujiombea mwenyewe na wanafunzi wenzako, ukimtumaini kwamba atakupa hekima, ujasiri, na nguvu za kutumia Neno lake katika maisha na huduma yako.

Ushauri na Maombi

MAZOEZI

Hakuna maandiko ya kukariri.

Kukariri Maandiko

4

Hakuna kazi ya kukabidhi.

Kazi ya Usomaji

Kufikia wakati huu unapaswa kuwa umeainisha mapendekezo yako kuhusu kile utakachofanya kwa habari ya Kazi ya Huduma na Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko, na mapendekezo hayo yawe tayari yamepitiwa na kuidhinishwa na mkufunzi wako. Hakikisha kwamba unapanga mambo yote mapema, ili usichelewe kutekeleza na kukusanya kazi zako. Mwishoni kutakuwa na mtihani wa kufanyia nyumbani, na utajumuisha maswali yaliyochukuliwa kutoka kwenye majaribio matatu ya kwanza, maswali mapya kutokana na maelezo ya somo hili, na maswali ya insha ambayo yatakutaka utoe majibu mafupi kwa maswali ya msingi yenye lengo la kuhusianisha somo na huduma na maisha. Pia, wakati wa mtihani, ni muhimu ujiandae kwa maswali ya kunukuu au kuandika mistari ya kukariri ya kozi hii. Utakapomaliza mtihani wako, tafadhali mjulishe mkufunzi wako na uhakikishe anapata nakala ya mtihani wako.

Kazi Nyinginezo

ukurasa 460  5

Taarifa Kuhusu Mtihani wa Mwisho

Made with FlippingBook - Online catalogs