Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
2 2 6 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Kama mwili wa Kristo ulimwenguni, Kanisa limeitwa kuwa mtetezi wa maskini, ambayo ni alama ya utume halisi wa Kikristo. Kuhusu utume wa mijini, Kanisa limeitwa kutangaza Habari Njema kwa maskini, hilo ni pamoja na kuwaheshimu kama walivyochaguliwa na Mungu na kama watu ambao Kristo alijitambulisha nao. Hatupaswi kamwe kuwadhalilisha, bali kushughulika nao kwa haki na huruma, tukiwa na uhakika kwamba wanaweza kugeuzwa na kuchangia katika maendeleo ya Ufalme. Hatutakiwi kukidhi mahitaji yao kijuujuu tu, bali kujitahidi kushughulika na mifumo na mahusiano kwa namna ambayo itachochea hali ya haki zaidi, yaani kuishi “Injili ya mafanikio” ya kweli, ambayo ni kutafuta haki na usawa kwa niaba ya walio hatarini zaidi miongoni mwetu. Ikiwa una nia ya kufuatilia baadhi ya mawazo ya somo hili la Utume wa Kikristo na Maskini , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Gordon, Wayne L. Real Hope in Chicago. Grand Rapids: Zondervan, 1995. Greenway, Roger S., ed. Discipling the City: A Comprehensive Approach to Urban Mission. 2nd ed. Grand Rapids: Baker Books, 1992. Perkins, John. With Justice for All. Glendale, CA: Regal Books, 1982. Phillips, Keith. No Quick Fix. Ventura, CA: Regal Books, 1985. Sherman, Amy L. Restorers of Hope: Reaching the Poor in Your Community with Church-based Ministries that Work. Wheaton, IL: Crossway Books, 1997. Sider, Ronald J. Just Generosity: A New Vision for Overcoming Poverty In America. Grand Rapids: Baker Books, 1999. Utawajibika sasa kutumia maarifa ya moduli hii kupitia mazoezi ya huduma kwa vitendo ambayo wewe na mshauri wako mtakubaliana. Matokeo ya dhana ya umaskini kwa utume wa Kikristo yako wazi. Hatupaswi kukosa ufahamu juu ya dhana muhimu kama hii, hasa kwa namna inavyohusiana na uhalali wa imani yetu. Katika kuwashirikisha wengine maarifa ya somo hili kupitia kazi yako ya huduma kwa vitendo utahitaji kufikiria kivitendo kuhusu jinsi mafundisho yako yavyonaweza kuathiri maisha ya ibada, maombi, na huduma ya kiroho uliyo nayo sasa hivi katika kanisa lako. Je, maarifa yaliyotolewa katika somo hili yanaweza kuathiri vipi mtazamo wako kazini, uhusiano wako na mwenzi wako au marafiki, au mtazamo wako kuhusu mahali unapoishi? Kinachofanya Neno kuwa hai katika maisha yetu ni uwezo wetu wa kuunganisha mafundisho na maisha yetu na huduma zetu. Kazi yako ya huduma ni fursa ya kutengeneza muunganiko
Nyenzi na Bibliografia
4
Kuhusianisha Somo na Huduma
Made with FlippingBook - Online catalogs