Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

4 3 6 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Kanisa, ameweka maagizo ya kuendea mbele. Kibinafsi na kwa pamoja, watu wote wa Mungu sasa wapo ulimwenguni kwa ajili ya kazi ya Mfalme. Kazi hiyo waliyopewa ina vipengele viwili vikuu. Kwanza, na kimsingi, ni kazi ya ushuhudiaji wa kimataifa, kufanya wanafunzi, na kuanzisha makanisa (Mt. 24:14; 28:19-20; Mk 13:10; Lk 24:47-48). Yesu Kristo ni lazima atangazwe kila mahali kama Mungu aliyefanyika mwili, Bwana, na Mwokozi; na mwaliko wa Mungu wenye mamlaka wa kupokea uzima kwa kumgeukia Kristo kwa toba na imani (Mt. 22:1-10; Lk 14:16-24) unatakiwa kutolewa kwa wanadamu wote. Huduma ya Paulo kama mpanda makanisa na mhubiri wa Injili kwa dunia yote kulingana na uwezo na mazingira yalivyomruhusu (Rum. 1:14; 15:17-29; 1 Kor. 9:19-23; Kol. 1:28-29) ni mfano bora wa kujitoa kwa kazi hii ya msingi. Pili, Wakristo wote, na vivyo hivyo kila kusanyiko la Kanisa duniani, wameitwa kuitenda kazi ya huruma na rehema, yaani upendo kwa jirani unaogusa mahitaji ya binadamu bila kusita katika kila namna yanavyojitokeza (Lk 10:25-27; Rum. 12:20-21). Huruma ilikuwa sehemu ya ndani ya upendo kwa jirani uliomsukuma Yesu kuponya wagonjwa, kulisha wenye njaa, na kufundisha wasiojua (Mt. 9:36; 15:32; 20:34; Mk 1:41; Lk 7:13), na wale waliopata kuwa viumbe wapya ndani ya Kristo lazima waonyeshe huruma hiyo hiyo. Kwa kufanya hivyo wanatimiza amri kuu ya pili na pia wanathibitisha kwa vitendo ukweli wa ujumbe wao kuhusu Mwokozi anayewageuza wenye dhambi kuwa wampendao Mungu na wanadamu wenzao. Ikiwa wale wanaohubiri ujumbe huu hawaionyeshi nguvu yake katika maisha yao wenyewe, ujumbe wao unakosa kigezo cha kuaminika. Lakini wakifanya hivyo, wanaufanya kuwa wa kuaminika zaidi. Hili ndilo Yesu alilolenga aliposema kwamba matendo mema ya mashahidi wake yatasababisha watu wamtukuze Baba yao aliye mbinguni (Mt. 5:16; cf. 1 Pet. 2:11-12). Matendo mema yanapaswa kuonekana ili kuunga mkono maneno mema. Vipengele hivi viwili—kuwa mashahidi kwa ulimwengu mzima na kutenda matendo ya huruma na rehema—vyote vinajengwa juu ya uelewa, hisia, na uzoefu wa nguvu ya simulizi ya Kikristo. Simulizi hii haipaswi kuonekana kama hadithi ya watoto tu, wala kama simulizi ya kubuni ya mtu anayejifanya wa kidini. Kwa Wakristo, hadithi ya Yesu wa Nazareti na kazi ya Mungu ndani yake na kupitia kwake ndiyo kweli halisi ya nyakati zote, tangazo pekee duniani ambalo linaweza ~ J. I. Packer. Concise Theology: A Guide to Historic Christian Beliefs . (toleo la kielektroniki). Wheaton, IL: Tyndale House Publishers, 1995.

Made with FlippingBook - Online catalogs