Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

/ 4 3 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

kumpa uzima wa milele kila anayeamini katika kweli yake na ahadi zake. Huu ndiyo msingi wa ushuhuda na chanzo cha matendo mema: simulizi la utukufu na upendo wa Mungu katika Yesu Kristo. Wazo la kuelewa elimu ya utume kama kusimulia hadithi linapaswa kuwapa tumaini wanafunzi wako wote wanaohisi wito wa huduma au utume (umisheni), lakini pengine hawajiamini kuwa wana vipawa vya kiakili vya hali ya juu au uwezo wa kuzungumza kwa ushawishi mkubwa. Ukristo kimsingi unahusu Mungu anayefanya kazi katika historia ya mwanadamu, na kazi hiyo imefika kwetu kupitia ushuhuda—simulizi la kazi hiyo na maana yake kwa wanadamu. Wote tunaweza kuelewa, kushirikisha, na kusimulia hadithi (ni kweli wengine hufanya vizuri zaidi ya wengine!). Wasaidie wanafunzi wako kufahamu urahisi na undani wa kweli hii kuu. Mitume hawakuwa wajumbe wa Yesu Kristo kwa sababu walikuwa na akili za kipekee au vipaji vya kipekee vya kuzungumza. Walikuwa mitume kwa sababu walikuwa mashahidi wa unyenyekevu wake, mateso yake, na utukufu wake. (2 Pet. 1:16 – “Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake”). Walimwona kwa macho yao wenyewe, na hivyo walikuwa na sifa ya kuwashirikisha wengine kile walichokiona na kukipitia. Huu ndio msingi na kiini cha huduma na utume. Tunapoutazama utukufu wake, tunabadilishwa ili kufanana naye, kutoka utukufu hadi utukufu, kwa Bwana, ambaye ni Roho (2 Kor. 3:18). Kisha tunakuwa katika nafasi ya kushirikisha wengine kile tulichokiona, tulichopitia, na tunachokijua kibinafsi (rejea 1 Yoh. 1:1-3). Simulizi inaendelea, nasi tunaendelea kuwa mashahidi wake kwa wengine. Maswali katika sehemu hii ya moduli yametolewa kwa ajili ya kurejea yaliyofundishwa, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wako wanaelewa kweli na maarifa muhimu yaliyofundishwa katika sehemu ya video. Katika sehemu hii ya kwanza, utahitaji kujadili na wanafunzi dhana ya utume kwa ujumla, na kisha kujadili mada mahsusi iliyogusiwa katika sehemu ya pili ya mafundisho ya video. Tafadhali panga muda wako vizuri. Kufanya mapitio ya masuala mapana kama haya kunaweza kuchukua muda mwingi, hasa iwapo wanafunzi wako watavutiwa na dhana hizo na kutamani kujadili kwa kina maana zake.

 4 Ukurasa 39 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook - Online catalogs