Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
4 3 8 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Utagundua pia kuna sehemu iliyoongezwa kwenye nyenzo hii inayohusu somo la missiolojia. Tafadhali soma sehemu hii pamoja na wanafunzi wako, na hakikisha kuwa wanaelewa kuwa missiolojia ni taaluma rasmi na elezea pia kuwa moduli hii ni aina ya missiolojia ya kimaandiko. Uelewa wao wa maneno ya kawaida yanayotumika katika uchambuzi wa kimaandiko na masomo ya kitheolojia ni muhimu, hasa kwa wale wanaotamani kuendelea na masomo ya masuala ya utume katika maeneo mengine. Kwa mara nyingine tena, tafadhali hakikisha muda unatosha kujadili hoja kuu vizuri, na kuwa na muda wa mapumziko kabla ya kuanza sehemu inayofuata ya video. Katika kila somo, unapewa orodha ya dhana kuu zilizofundishwa katika somo hilo. Hii ni sehemu yenye msaada mkubwa, kwa ajili yako na kwa wanafunzi wako, katika kupitia maarifa muhimu ambayo maudhui ya somo yalilenga kufundisha. Dhana hizi zimeandikwa kwa njia ya muhtasari ili kuonyesha kwa ufupi taarifa mbalimbali zilizojadiliwa katika somo, kwa kuzingatia zaidi sehemu ya video na majadiliano uliyoyaongoza pamoja nao. Wakumbushe wanafunzi jinsi sehemu hii ilivyo na manufaa makubwa, si tu kwa ajili ya kupitia yaliyofundishwa, bali pia kwa ajili ya maandalizi ya majaribio na mtihani watakaofanya katika kozi hii. Moja ya stadi kuu tunazotarajia kuwafundisha wanafunzi wetu ni uwezo wa kuwa wawazi na wa kweli kwa kina kuhusu maisha yao binafsi, na namna ya kutumia kweli za Biblia katika hali halisi ya maisha yao ya kila siku katika kutembea na Kristo. Ili kuwasaidia kujifunza ujuzi huu, sehemu hii imewekwa katika kila moduli ya kozi ya Capstone. Sehemu hii imebuniwa mahsusi kuwasaidia wanafunzi kukabiliana moja kwa moja na kile ambacho wanajifunza katika somo fulani na namna wanavyoweza kutumia maarifa ya somo hilo katika maisha yao binafsi. Unapowaongoza katika jitihada hii, unaweza pia kuwapa mfano kwa kuzungumzia jinsi unavyoona kweli hizi zikigusa maeneo mbalimbali ya maisha yako. Zaidi ya hayo, unaweza kubuni maswali yako mwenyewe ili “kuwasha moto” wa hamasa ndani yao. Kilicho muhimu zaidi ni kuhakikisha tunatumia muda huu si kwa kurudia tu taarifa, bali kufikia kiini cha yale wanayofikiri, wanayohisi, na
5 Ukurasa 55 Muhtasari wa Dhana Muhimu
6 Ukurasa 58 Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi
Made with FlippingBook - Online catalogs