Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
/ 4 3 9
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
wanayochagua katika maisha yao binafsi, na jinsi kweli za somo hili zinavyoweza kugusa mawazo yao, hisia, na maamuzi yao. Hulazimiki kufanyia kazi kila swali lililoandikwa hapa chini, au kuyajibu kimazoea. Lengo letu ni kuwa na mazungumzo ya wazi na wanafunzi kuhusu maisha yao na mioyo yao, na kuangazia masuala, changamoto, maswali, na mawazo yanayotokana moja kwa moja na matukio fulani ndani ya maisha yao, na yanayohusiana na maisha yao na huduma zao kwa ujumla. Usisite kutumia muda mwingi kwenye swali lililoibuka kutokana na video, au linalohusiana sana na huduma wanazofanya kwa sasa. Lengo la sehemu hii ni kuwawezesha kufikiri kwa kina na kwa mtazamo wa kitheolojia kuhusu maisha yao na muktadha wa huduma zao. Kwa mara nyingine tena, maswali yaliyopo hapa chini yamewekwa kama miongozo na vichocheo vya fikra, na hayapaswi kuonekana kuwa ya lazima. Chagua baadhi ya maswali, au tengeneza ya kwako mwenyewe. Jambo kubwa hapa ni kuona kwamba mambo yanayojadiliwa ni ya muhimu kwa wanafunzi sasa, kwa muktadha wao kihuduma na yanaleta majibu kwa maswali yao. Moja ya majukumu yako kama mshauri ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wako wanafahamu mahali mlipofikia katika kozi mnayojifunza, ni dhana zipi mnazojifunza kwa sasa na zipi zitafuata, pamoja na kazi (kama zipo) ambazo wanatarajiwa kukamilisha hivi karibuni. Hakikisha wanaelewa vizuri kazi ya darasa lijalo, ikiwemo jaribio lijalo na muhtasari wa kazi ya kusoma. Kwa upande mwingine, kazi ya kusoma ni muhimu, lakini haikukusudiwa kuwa ngumu; lengo lake ni kuwahimiza kusoma kile walichopewa kwa uwezo wao wote, na kisha kuandika sentensi chache kueleza kile ambacho wameelewa kutoka kwenye kitabu hicho. Huu ni ujuzi muhimu wa kiakili kwao kujifunza, hivyo hakikisha unawatia moyo katika mchakato huo. Bila shaka, kwa wanafunzi ambao watakutana na ugumu, wahakikishie kuhusu kusudi la kazi hiyo—weka mkazo kwamba uelewa wa kile wanachokisoma ndio jambo la msingi na sio uwezo wao wa kuandika. Tunataka kuboresha ujuzi wao, lakini si kwa gharama ya kuwavunja moyo au kuwazuia kujifunza. Hata hivyo, hatupaswi pia kuwapunguzia viwango vya matarajio. Hapa, tafuta uwiano sahihi kati ya kuwapa changamoto na kuwahamasisha.
7 Ukurasa 63 Kazi
Made with FlippingBook - Online catalogs