Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

/ 4 4 1

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo: Sehemu ya 2

MAELEZO YA MKUFUNZI 2

Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi, Somo la 2 : Maono na Msingi wa Kibiblia wa Utume wa Kikristo – Sehemu ya 2 . Lengo kuu la somo hili ni kufuatilia wazo la hadithi ya mapenzi ya kiungu na vita kati ya falme kama mada mbili kuu za Maandiko Matakatifu zinazotoa maana pana na ya msaada katika kuelewa utume (umisheni). Wazo kuu la moduli hii ni kwamba umisheni hauwezi kupunguzwa kuwa aina fulani ya uinjilisti, mbinu ya huduma mijini, au seti ya huduma zinazolenga kukidhi mahitaji ya wengine. Umisheni unajumuisha mambo haya na mengine mengi ya ushuhuda na matendo mema, lakini kiini cha umisheni ni mwendelezo wa tamthilia ya kiungu—mapenzi, vita, na ahadi. Tunasisitiza kwamba elimu ya kweli ya umisheni huanzia kwenye hadithi ya Maandiko kuhusu Mungu na watu wake, Mungu na uumbaji wake, na kutoka kwenye mtazamo huu salama ndipo tunaanza kupata muundo, mguso, na mwelekeo wa shughuli na wito au shauku zetu za kimisheni. Umisheni unaotokana na jitihada za kibinadamu peke yake, si wa kibiblia kwa maana halisi. Ili umisheni uongozwe na Bwana, lazima uanze na kusudi la Bwana, moyo wake, na kazi yake—ile kazi ya ukombozi ambayo kilele chake kiko katika Yesu wa Nazareti na huduma yake. Chochote kilicho pungufu ya hapo si umisheni wa kweli. Kwa kweli, ili kuelewa umisheni (au eneo lolote muhimu la theolojia na elimu ya umisheni) ni lazima kujifunza namna waandishi waliovuviwa na Roho walivyotumia picha, mafumbo, alama, na simulizi. Kupitia matumizi ya kiungu ya fikra na taswira, waandishi wa Biblia walitufunulia mpango na kusudi la Mungu. Uwezo wetu wa kufuata mawazo yao na kugundua mantiki yao hautawezekana iwapo tutapuuza nguvu ya matumizi ya fikra za Kikristo (na zilizo chini ya mwongozo wa Maandiko). C. Seerveld analieleza jambo hili kwa uwazi: Dhana ya Kikristo ya kibiblia ya mawazo itatofautisha kati ya kuwaza kwa msingi wa makosa ya kimtazamo, kwa msingi wa picha au taswira, na kuwaza kama ufunuo wa neno la kweli. Shughuli ya ubunifu ya binadamu ni tofauti kabisa na hisia au kufikiri kwa kawaida, lakini pia ni shughuli ya kweli inayohusiana na utendaji kazi wote wa binadamu. Kuwaza ni zawadi ya Mungu ambayo kwayo wanadamu huweza kuamini mambo. Kwa uwezo wa kuwaza mtu hujiaminisha na kutenda “kana kwamba hiki… ni kile…” (k.m. Mungu ni mwamba, Isa. 17:10; Kristo ni bwana-arusi, Mt. 25:1 13). Mawazo ya mwanadamu ndio chanzo cha maarifa ya sitiari na ucheshi ambavyo ni muhimu sana kwa mtindo wa maisha wa mtu yeyote. Kuwaza kunakusudiwa kuwa

 1 Ukurasa 67 Utangulizi wa somo

Made with FlippingBook - Online catalogs