Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

4 4 4 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Ibada hii inazingatia wazo la mapenzi ya kiungu, kwa kuangazia karamu ya ndoa ya Mwanakondoo kama ilivyotajwa katika Ufunuo 19. Wazo la ndoa kama njia ya kuelezea uhusiano wa Mungu na watu wake, pamoja na mwaliko kwa wote kuja na kuwa sehemu ya kundi hilo linalounda bibi-arusi wa Kristo, ni mada kuu katika ufunuo wa kibiblia. R. C. Ortlund Jr. anazungumzia taswira hii ya Kristo kama bwana-arusi na mume wa watu wa Mungu, yaani Kanisa, wakati wa ukamilifu wa mambo yote kama ilivyoelezwa katika maandiko ya mwisho ya kitabu cha Ufunuo. Akitoa maoni kuhusu mandhari yanayoonyeshwa mbinguni baada ya kuangamizwa kwa kahaba mkuu, Babeli, Ortlund anaeleza kwamba: Baada ya Babeli, “kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake” (Ufu. 19:2), kuhukumiwa na Mungu, watakatifu waliopata ushindi wanashangilia kuwa ndoa ya Mwanakondoo imewadia, na bibi-arusi wake amejiandaa (Ufu. 19:7). Amepewa neema ya kuvikwa “kitani nzuri, ing’arayo, safi,” ambacho ni matendo ya haki ya watakatifu (Ufu. 19:8). Bwana-arusi wa bibi-arusi analileta Kanisa kwake mwenyewe katika fahari, pasipo doa, kunyanzi au kitu chochote cha aina hiyo (taz. Efe. 5:26-27). Uhalisia wa mfano wa zamani unaonekana hatimaye pale Yerusalemu mpya inaposhuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ikiwa imejiandaa kama bibi-arusi aliyepambwa kwa ajili ya mume wake (Ufu. 21:2). Hakutakuwa na ndoa za kibinadamu mbinguni (Mk 12:25), kwa maana mbingu yenyewe itakuwa ndiyo ndoa. Ni vigumu kulizungumzia hili bila kutumia lugha ya juu sana, kama Jonathan Edwards anavyoonyesha (*Works [Edinburgh, 1979 rudio], tol. 2, uk. 22): Ndipo Kanisa litaletwa kwenye furaha kamili ya kuwa na bwana-arusi wake, machozi yote yakiwa yamefutwa kutoka machoni pake; na hakutakuwa tena na umbali wala kutengana. Ataingizwa kwenye karamu ya harusi ya milele, na kukaa milele na bwana arusi wake; naam, akae milele katika kumbatio lake. Ndipo Kristo atampa mapenzi yake; naye atakunywa hadi ashibe, naam, ataogelea katika bahari ya mapenzi yake. Hitimisho: muundo wa jumla wa mafundisho ya kibiblia kuhusu ndoa unaonyesha ulinganifu wa mfano kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo, ambapo “umoja wa mwili mmoja” katika ndoa ya kibinadamu, ambayo ni takatifu lakini ya muda, unaelekeza mbele na juu zaidi kwenye muungano wa kiroho wa milele kati ya Kristo na bibi-arusi wake, yaani Kanisa. Ishara iliyomo katika ndoa ya duniani inaupa uhusiano huo heshima kuu; kina

 2 Ukurasa 69 Ibada

Made with FlippingBook - Online catalogs