Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

/ 4 4 3

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo” (Kol. 2:15). Katika Waefeso 4:8 ananukuu wimbo wa shujaa wa kiungu kutoka Agano la Kale (Zab. 68) na hivyo kutazama kupaa kwa Kristo kama gwaride la ushindi: “Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.” Hivyo basi, taswira ya shujaa wa kiungu inatumika katika Agano Jipya kuelezea ushindi wa Yesu dhidi ya Shetani msalabani. Ingawa Shetani ameshindwa, Agano Jipya linaelewa pia kwamba kwa muda bado anaweza kusababisha mateso makubwa. Kipindi kilichopo kati ya kazi ya msalaba wa Kalvari na kurudi kwa Kristo ni kipindi kati ya vita vilivyoleta ushindi wa mwisho na kushindwa kabisa kwa Shetani na mwisho wa uhasama. Katika kipindi hiki, vita vinaendelea, na kanisa limeagizwa kupigana dhidi ya maadui wa Mungu kama Israeli walivyokuwa jeshi la Mungu katika Agano la Kale. Tofauti ni kwamba silaha za kanisa ni za kiroho, si za kimwili (taz. Efe. 6:10-20). ~ Leland Ryken. The Dictionary of Biblical Imagery . (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. p. 213. Kazi yako katika moduli hii ni kuwasaidia wanafunzi kuelewa vizuri taswira hizi kama zilivyotumiwa na waandishi wa Biblia, na kuzitumia kama lenzi ya kuwawezesha kupata mtazamo mpya kuhusu asili ya umisheni wa Kikristo kama inavyoonekana kupitia taswira hizi . Namna hii ya kufikiri, mtazamo huu wa kutafsiri Maandiko ni msaada mkubwa katika kufunua utajiri na nguvu ya umisheni wa Kikristo leo, na pia kulinda umisheni usipunguzwe kuwa mbinu za kiufundi tu au sheria za utekelezaji. Wasaidie wanafunzi wako kupata hisia za mafumbo haya na taswira zake—furaha ya karamu ya harusi, na shangwe ya kushindwa kwa adui. Taswira hizi hazikutolewa kwa ajili ya maarifa tu, bali kwa ajili ya moyo na nafsi; wawezeshe wanafunzi wako kufikiri kwa uwazi, lakini pia wafundishe kuhisi kwa undani kupitia taswira hizi, kwa kuwa ndiyo sababu Bwana alitupatia zawadi hii ya picha na mafumbo. Tafadhali angalia tena malengo yaliyoainishwa hapa chini, na kumbuka jinsi yanavyokuwa na nafasi ya kipekee katika kila kipengele cha mafundisho darasani. Kwa mara nyingine tena, mojawapo ya majukumu yako muhimu kama Mkufunzi ni kusisitiza dhana hizi wakati wote wa somo, hasa wakati wa mijadala na muda wote uwapo pamoja na wanafunzi. Kadri utakavyoweza kuonyesha umuhimu wa malengo haya katika kipindi chote cha darasa, ndivyo wanafunzi watakavyoweza kuelewa na kufahamu uzito na ukubwa wa malengo haya.

Made with FlippingBook - Online catalogs