Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
/ 4 4 7
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Utume wa Kikristo na Jiji
MAELEZO YA MKUFUNZI 3
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi, Somo la 3, Utume wa Kikristo na Jiji . Mtazamo wa jumla wa somo hili ni juu ya umuhimu wa jiji katika utume, ukijengwa juu ya mtazamo wa kibiblia na wa kieksejesia kuhusu jiji. Kama ilivyoonyeshwa katika moduli hii kwa ujumla, tunalenga kuwapa wanafunzi msingi mpana na wa kibiblia kuhusu Utume wa Kikristo ambao utawasaidia kuelewa vipengele vya utume kwa mwanga wa picha nzima. Yaani, dhamira yetu ni kuona kazi ya Mungu ulimwenguni katika historia, kisha, kwa kadiri tuwezavyo, kuelewa nafasi na upeo wa utume katika muktadha wa historia hiyo. Hili linahitaji tuendelee kuwa na mtazamo wa “picha kubwa” badala ya kupotea katika kipengele chochote cha utume, hata kama ni muhimu kiasi gani. Wazo la jiji na jukumu letu la kutoa ushuhuda wa kinabii kwa jiji, pamoja na kutenda haki na rehema ndani yake, linatokana na uelewa wetu wa utume wa Kanisa kwa ujumla. J. A. Kirk anatoa muhtasari wa kina wa kile anachoamini kuwa ni majukumu ya Kanisa katika utume, kwa kuzingatia theolojia ya utendaji wa Mungu katika ulimwengu tunaoukabili: Utume wa Kanisa unaweza kujumlishwa katika kazi tano za jumla. Mpangilio ambao zimeorodheshwa hapa chini haukusudiwi kuonyesha vipaumbele katika umuhimu wake. Kuzungumza kibiblia, kila kipengele hapa ni cha muhimu sana. Kwa kukazia kipengle kimoja zaidi kuliko nyingine, vikundi mbalimbali vya Wakristo vimeelekea kuona baadhi ya vipengele hapa kama mambo ya ziada. Hata hivyo, Mungu haruhusu hilo! 1. Ni kuhusika katika kusimamia rasilimali za uumbaji . Hii ina maana ya kuhimiza matumizi yenye hekima na uwiano ya uumbaji wa asili wa Mungu, kwa kujihusisha katika vipengele vingi vya uhifadhi na kutokomeza uchafuzi wa mazingira. Kanisa litaelekeza watu kwenye kuheshimu na kuthamini zawadi ya Muumba ya uhai kwa wote ambayo ina maana ya kupinga uchoyo na ubinafsi, na kuhimiza kuwa na kiasi katika matumizi ya rasilimali kwa wote kwa njia ambayo vizazi vijavyo vitaweza kuishi maisha yenye ustawi endelevu duniani. 2. Ni kuwahudumia wanadamu bila ubaguzi na kwa mahitaji yao yoyote . Kanisa lina kazi ya huruma ya kuwasaidia wakimbizi na wahanga wa ukame na njaa na kusaidia kuanzisha miradi ya maendeleo, kampeni za kusoma na kuandika, elimu ya afya na programu za makazi. Lina jukumu maalum la kuhudumia mahitaji ya walemavu, wazee, waliofiwa, watoto wa
1 Ukurasa 123 Utangulizi wa somo
Made with FlippingBook - Online catalogs