Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
/ 4 5 1
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Yerusalemu ina umuhimu wa pekee kwa manabii kama kituo cha kidini cha nchi takatifu baada ya urejesho (Eze. 45:1-6). Yahweh ameliweka jina lake juu ya Mlima Sayuni, na mji huo utapokea zawadi na ibada kutoka kwa mataifa mengi (Isa. 18:7; Zek. 8:22-23). Kwa njia hii, Yerusalemu inawakilisha watu wa Mungu, ambao watafurahia wokovu wa Mungu baada ya kipindi cha kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao. Neno la Mungu litatoka Yerusalemu (Isa. 2:3); watu watakusanyika kumheshimu (Yer. 3:17); na mfalme wa masihi ataonekana kwa ushindi (Zek. 9:9-10). Haieleweki daima ni katika muda gani hasa unabii huu wa wokovu utatimia; baadhi ya ahadi zinaelekea kwenye siku za mbele sana. Katika enzi ijayo, utawala wa Yahweh utaimarishwa kabisa Yerusalemu (Isa. 24:23; 65:18-19). Yerusalemu hatimaye litakuwa jiji takatifu na halitashindwa tena na mataifa ya kigeni (Yoeli 3:17). Katika vifungu hivi vya kinabii, Yerusalemu imekuwa zaidi ya kituo cha kisiasa. Sasa inatumika kama ishara ya kilele na utimilifu wa mwisho wa mpango wa wokovu wa Yahweh [msisitizo ni wangu]. ~ B. T. Arnold. “City.” The New Dictionary of Biblical Theology . T. D. Alexander, ed. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2001. Namna, upeo, na kusudi la mabadiliko haya ya jiji — kutoka kuwa jiji la uasi hadi kuwa ishara ya utimilifu wa mwisho wa mpango wa wokovu wa Mungu — ndilo kusudi kuu la somo hili na ibada hii. Ukweli kwamba Mungu mwenyewe alibadilisha mtazamo wake kuhusu jiji una maana ya kina sana kwetu leo, hasa tukizingatia ukweli kwamba watu wengi zaidi sasa hivi wanaishi mijini kuliko maeneo mengine yoyote duniani. Miji imekuwa kitovu cha mamlaka, biashara, serikali, na jeshi kwa mataifa yote makubwa duniani, na mamilioni ya watu maskini zaidi duniani leo wanahamia mijini kwa idadi ambayo haijawahi kushuhudiwa kabla. Kwa hakika, huu ni wakati wa Wakristo walioangaziwa na wanaoelewa Maandiko kwa kina kuutathmini upya ujumbe wa Biblia kuhusu jiji, na kujipanga upya ili kusimama katika utume wa Mungu ndani ya miji na majiji yetu. Angalia mwishoni mwa maswali yafuatayo kuna nukuu ndefu kutoka kwa Profesa Ryken kuhusu maana ya theolojia ya jiji katika maisha ya Kikristo. Hakikisha unasoma sehemu hii pamoja na wanafunzi, na uongoze majadiliano juu ya maana ya jiji kwa waamini. Kwa namna fulani, Ryken anaweka msingi akisema kwamba haijalishi mtu anaishi mjini au la, bado ameunganishwa kwa njia ya msingi na
3 Ukurasa 142 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook - Online catalogs