Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
4 5 2 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
dhana ya jiji takatifu, Yerusalemu Mpya, na hili kwake lina athari za moja kwa moja kwa mwenendo wetu wa Kikristo na huduma zetu. Baada ya kupitia mada kuu katika sehemu ya kwanza ya video, pitia nukuu hii pamoja na wanafunzi.
Angalia mwisho wa maswali yafuatayo kuna nukuu ndefu kutoka kwa J. A. Kirk kuhusu majukumu ya Kanisa. Pitia kwa ufupi majukumu haya kwa kuzingatia kile ambacho mmekigundua katika video kuhusu tabia za miji ya kisasa duniani. Wasaidie wanafunzi wako kuelewa jukumu la kiumisheni la Kanisa kwa kuzingatia na kwa kuunganishwa na hali halisi ya miji ya kisasa — wanaamini nini kuhusu umisheni na mji kwa kuzingatia ushuhuda wa Maandiko kuhusu hilo? Pitia nukuu hiyo kwa haraka pamoja na wanafunzi, kisha jadilini uchambuzi wake kwa pamoja baada ya kupitia hoja kuu zilizotolewa katika sehemu ya kwanza ya video. Sasa umesalia na somo moja tu kukamilisha kozi ya Misingi ya Utume wa Kikristo . Ifikapo mwisho wa kipindi cha pili cha darasa, unapaswa kusisitiza kwa wanafunzi umuhimu wa kuwa tayari na kuwa wamefanya maandalizi ya kina kuhusu jinsi wanavyokusudia kutekeleza Kazi yao ya Huduma. Vilevile, kufikia wakati huu, unapaswa kuwa umesisitiza juu ya uchaguzi wa vifungu vya Maandiko ambavyo watafanyia kazi kwa ajili ya Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko. Kazi hizi zote mbili zitafanyika kwa ubora na kwa mawazo ya kina ikiwa wanafunzi wataanza kuzifikiria na kufanya maamuzi mapema. Usishindwe kusisitiza hili, kwa kuwa, kama ilivyo kwa masomo mengine yote, mwishoni mwa kozi mambo mengi huwa yanatakiwa kukamilishwa kwa wakati mmoja, na wanafunzi huanza kuhisi shinikizo la kukamilisha kazi mbalimbali kwa wakati mmoja. Kwa sababu hii, tunashauri pia kwamba ufikirie kupunguza alama kidogo kwa kazi au mitihani inayowasilishwa kwa kuchelewa. Ingawa kiwango cha upunguzaji kinaweza kuwa kidogo, utekelezaji wa sheria zako utawasaidia kujifunza kuwa na ufanisi na kuwa waaminifu wa muda wanapoendelea na masomo yao.
4 Ukurasa 161 Maswali kwa Wanaunzi na Majibu
5 Ukurasa 173 Kazi
Made with FlippingBook - Online catalogs