Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
/ 4 5 3
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Utume wa Kikristo na Maskini
MAELEZO YA MKUFUNZI 4
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi, Somo la 4, Utume wa Kikristo na Maskini . Somo hili la mwisho katika moduli yetu ya Misingi ya Utume wa Kikristo linahusu nafasi na umuhimu wa maskini katika muktadha wa utume wa Kikristo. Mada ya watu maskini badala ya kuwa maelezo ya ziada katika ujumbe wa Injili, tunalenga kuonyesha kwamba suala la maskini ni sehemu ya msingi ya utume, kama vile utume ulivyo sehemu ya msingi ya Kanisa. Kuhusu utume na Kanisa, Kirk anafafanua kwa uwazi kwamba asili ya kiroho, kwa kuzingatia agizo kuu, ni kwenda, kuendelea kwenda, na kutumwa. Neno ‘utume’ linabeba dhana ya kibiblia ya ‘kutumwa,’ ambayo imeonyeshwa kwa ufasaha katika maneno ya Yesu: ‘kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi’ (Yohana 20:21). Mlingano kati ya Mungu kumtuma Yesu na Yesu kuwatuma wanafunzi wake unaelezea njia na kiini cha utume. Hivyo basi, utume wa kanisa unahusisha kila kitu ambacho Yesu aliwatuma watu wake wakafanye ulimwenguni. Haimaanishi kila jambo ambalo kanisa linafanya au kila jambo ambalo Mungu analifanya duniani. Kwa hiyo, kusema kuwa kanisa lenyewe ni utume ni kupitiliza. Hata hivyo, kupuuza au kulegeza agizo la kwenda ulimwenguni kote kama wawakilishi wa Yesu kunaonyesha maisha yenye upungufu wa kiroho. ‘Kanisa linaishi kwa utume kama vile moto unavyoishi kwa kuwaka.’ ~ J. A. Kirk. “Missiology.” The New Dictionary of Theology . S. B. Ferguson, ed. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 435. Ikiwa Kirk yuko sahihi kwa kusema kwamba “kanisa linaishi kwa utume kama moto unavyoishi kwa kuwaka,” basi kanisa linapaswa kuwaka kwa ajili ya nani , na kwa kusudi gani ? Je, Mungu anatoa mwanga wowote kuhusu kundi maalum, shabaha, au watu ambao angependa utume wake uwalenge kwa dhati? Kwa kuwa Injili ni kwa ajili ya ulimwengu mzima (taz. Yoh. 3:16; 1 Yoh. 2:12), je, si itakuwa upendeleo au ubaguzi kusema kwamba kundi fulani linazingatiwa au kujaliwa zaidi na Mungu kuliko makundi mengine? Je, hilo halitoi picha mbaya kuhusu haki kamilifu ya Mungu na asili yake ya kutokuwa na upendeleo? Maswali haya na mengine yanayohusiana nayo yamekuwa yakisumbua akili za waumini waaminifu na wacha Mungu, ambao wamefikia hatua ya kutofautiana kuhusu asili ya majibu ya maswali hayo. Kwa upande mmoja, wapo wanaotetea kwa nguvu kwamba kutokupendelea kwa Mungu kunazuia mjadala wowote kuhusu uwepo wa “chaguo la kipaumbele kwa maskini” katika kazi ya Mungu;
1 Ukurasa 177 Utangulizi wa somo
Made with FlippingBook - Online catalogs