Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

4 5 4 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

kwamba Mungu lazima awajali watu wote kwa usawa ili aendelee kuwa Mungu asiye na upendeleo. Kwa upande mwingine, hata hivyo, kuna msururu wa ufunuo na hoja katika Maandiko unaoonyesha mzigo mzito na dhamira ya Mungu kwa ajili ya maskini na waliokandamizwa. Katika karne ya 20, fani nzima ya utafiti wa kitheolojia (theolojia ya ukombozi) imejitolea kuchunguza uhusiano kati ya wokovu na ukombozi wa Mungu na wale walio hatarini zaidi—waliokandamizwa, waliotengwa, na waliodhulumiwa. Vita vya kitheolojia bado vinaendelea kwa nguvu, na mijadala yetu katika somo hili haitakuwa kamwe neno la mwisho na hitimisho la mada hii nyeti na muhimu. Ingawa hatutatoa neno la mwisho, tunatumaini kwamba mjadala wetu utawafanya wengi kutafakari upya ushahidi mzito wa kibiblia unaoashiria kwamba Mungu anajitambulisha moja kwa moja na mateso ya maskini na wale waliomo katika muktadha wao (yaani, wajane, yatima, wageni, wahamiaji, waliokandamizwa, n.k.). C. M. N. Sugden anazungumzia namna Bwana anavyoshughulikia “upotovu” katika jamii ya wanadamu uliosababishwa na dhambi, na anasema kuwa kazi ya Mungu katika hali kama hizi daima huanza na wale wanaoteseka kwa undani na wenye uchungu zaidi kutokana na tamaa mbaya, ubinafsi, na ukandamizaji unaotokana na upotovu huo: Wakati Mungu anaposhughulikia upotovu ulioletwa na dhambi ya mwanadamu duniani, anaanza na wale wanaoteseka kwa kina zaidi kutokana na tamaa mbaya, ubinafsi, na matumizi mabaya ya mamlaka juu ya wengine—wafanyakazi wahamiaji wa Kiebrania waliokuwa Misri. Aliwakomboa kutoka katika ukandamizaji wa Farao. “Wape watu wangu ruhusa waende ili waniabudu” (Kut. 3-5). Ukombozi wa Mungu kwa Israeli uliweka wazi na kueleza kile ambacho alikuwa akikifanya duniani (Kum. 26:1-10). Ulifunua baadhi ya nyanja za uasi dhidi ya Mungu, kwa mfano, ukatili wa Farao. Ulionyesha yale ambayo Mungu anayajali—kwamba watu wote kwa pamoja wawe wasimamizi wa rasilimali za dunia (Mwa. 1:27-28; Kut. 3:8). Ulionyesha namna Mungu anavyofanya kazi duniani kuleta ukombozi—kwa kuchagua kile kilicho duni, ili kuaibisha majivuno ya wanadamu (Kum. 7:7-8; 1 Kor. 1:21-31). ~ C. M. N. Sugden. “Poverty and Wealth.” The New Dictionary of Theology . S. B. Ferguson, ed. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 523.

Made with FlippingBook - Online catalogs