Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
4 5 6 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Wasamaria, wale waliotajwa kuwa ‘wenye dhambi,’ na waliokataliwa kijamii. Huduma yake haikufungiwa kwao tu, lakini alibainisha asili yake kupitia wao; kutangaza kwake Injili na matendo yake ilikuwa habari njema kwa maskini (Luka 4:18; 7:22). Maana ya huduma ya Yesu miongoni mwa maskini ndiyo iliyotoa maana ya kile alichokuwa akifanya kwa watu wengine wowote. Umuhimu wa habari njema kwa matajiri ulipaswa kuonekana kupitia kile ambacho Yesu alikuwa akifanya miongoni mwa maskini. Jinsi mtoza ushuru (maskini kijamii) alivyopokea msamaha ndiyo ilipaswa kuwa kielelezo cha jinsi Farisayo anavyopaswa kuupokea (Luka 18:9-14), si kinyume chake. Hivyo basi, habari njema ya Injili kamili ya Ufalme inapaswa kuletwa kwa jamii nzima kupitia maskini. Jinsi jamii inavyowatendea maskini wake ndicho kipimo kikuu cha maisha ya jamii hiyo, kwa mujibu wa Biblia (Yak. 2:1-7). Na njia ambayo jamii hubadilishwa ni kupitia maskini. Katika Biblia, neema ya Mungu kwa ujumla inapatikana kwa wote kwa usawa. Lakini katika Agano la Kale, uhalisia na asili ya neema hiyo vinafunuliwa kupitia kile ambacho inamaanisha kwa Israeli. Agano la Kale linazingatia zaidi jinsi neema hiyo inavyodhihirika katika mahusiano ya kiuchumi (taz. Law. 25). Katika Agano Jipya, maskini wanachukua nafasi ya Israeli kama kiini cha Injili. Kadri maskini wanavyoipokea habari njema ya Ufalme, asili halisi ya Injili hujidhihirisha kwa wengine. Agano Jipya linatoa mkazo maalum kuhusu maana ya Injili kwa kuielekeza kwa watoto, wanawake, Wasamaria, waliotengwa kijamii, wagonjwa, na “kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.” ~ Ibid., uk. 523-524. Moduli hii inashughulikia moja kwa moja msisitizo huu katika jamii ya Agano la Kale, pamoja na maisha na huduma ya Yesu, na agizo lake kwa Kanisa lake. Uchanganuzi wa Sugden kuhusu maskini kusimama katika nafasi inayofanana na ya Israeli ni uchambuzi wenye kina cha ufahamu na ninaamini ni uchambuzi unaoweza kutetewa kwa msingi wa utafiti wa maandiko ya Biblia kuhusiana na somo hili muhimu. Ingawa kuna nafasi kubwa ya kutia chumvi, kuchanganyikiwa, na kuweka msisitizo mkubwa juu ya mada fulani bila kujumuisha zingine, naamini tutaona uhusiano muhimu uliopo kati ya masikini na utume wa Kikristo. Kwa kuzingatia aina za mikanganyiko inayowezekana kutokea katika mjadala kama huu, itakuwa muhimu sana kwako kuwa tayari kikamilifu kuongoza na kuwezesha majadiliano yanayozingatia malengo yaliyo hapa chini. Hakikisha kwamba unapitia malengo haya kabla ya somo, kwamba unaelewa maelezo yaliyomo katika malengo
Made with FlippingBook - Online catalogs