Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

/ 4 5 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

haya, na uko tayari kabisa kuyajadili na wanafunzi baada ya sehemu za video. Eneo hili limebeba mawazo mengi na mazito, na malengo haya yanaweza kukupa mwelekezo mzuri kuhusu dhana ambazo ungependa kuangazia na kuwekeza mkazo zaidi unapoendelea na somo.

Ibada hii inazingatia uthibitisho wa umasihi wa Yesu kulingana na namna anavyowatendea watu, uponyaji na utunzaji, na ujumbe wake kwa maskini. Kwa maneno mengine, tukio hili linafunua ukweli kwamba Yohana Mbatizaji angeweza tu kujua kwa uthabiti na kwa uwazi kwamba Yesu wa Nazareti alikuwa hakika Masihi kwa sababu ya aina za matendo aliyoyafanya katika uhusiano wake na watu waliokuwa maskini zaidi, waliokuwa hatarini zaidi, na watu waliotengwa katika Israeli. Upendo wake na utunzaji wake kwao ulikuwa uthibitisho wa kutosha kwamba kwa kweli alikuwa Masihi kwa kuzingatia matendo yake ya kimiujiza kati yao. Kinachoendelea katika kifungu hiki kizima ni dhana ya Yesu kwamba Yohana hakika angetambua matendo haya na ujumbe wake wa ukombozi kwa maskini kama ishara na uthibitisho wa utambulisho wake kama mpakwa mafuta wa Mungu. Tumaini la Israeli lilihusishwa moja kwa moja na tazamio na ujio wa Mfalme na Mtawala ambaye angerudisha haki na uadilifu miongoni mwa jamii ya agano ya Bwana. Hapa kuna sampuli wakilishi chache za baadhi ya maandiko muhimu ya Kimasihi ambayo yana maana hii ya haki na amani inayohusishwa na ujio wake: Isa. 11:1-10 – Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda. 2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana; 3 na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake; 4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya. 5 Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia. 6 Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza. 7 Ng’ombe na dubu watalisha

 2 Ukurasa 180 Ibada

Made with FlippingBook - Online catalogs