Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

/ 4 5 9

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo. Zab. 45:4-6 - Katika fahari yako usitawi uendelee Kwa ajili ya kweli na upole na haki Na mkono wako wa kuume Utakufundisha mambo ya kutisha. 5 Mishale yako ni mikali, watu huanguka chini yako; Imo mioyoni mwa adui za mfalme. 6 Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele, Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. Isa. 61:1-4 - oho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao; 3 kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe. 4 Nao watajenga mahali pa kale palipoharibiwa, watapainua mahali palipokuwa ukiwa zamani, watatengeneza miji iliyoharibiwa, mahali palipoachwa kizazi baada ya kizazi. Andiko hili la mwisho, kama unavyoweza kukumbuka, ni lile andiko la Agano la Kale ambalo Yesu alisoma katika mahubiri yake ya uzinduzi wa huduma yake huko Nazareti akitangaza utambulisho wake kama Masihi (taz. Lk 4:16-18). Kinachoonekana wazi kutokana na sampuli hii ya maandiko ni kwamba Biblia iko wazi kwamba kuja kwa Masihi kungehusisha kuja kwa uadilifu na haki kwa maskini na waliokandamizwa. Kuja kwa Mtiwa-mafuta wa Mungu kungeleta utawala wa amani, uhuru, ukamilifu, na haki, na kungewakilisha mwisho wa uonevu na kutengwa. Ibada hii inakazia uhakika wa utambulisho wa Yesu kama Masihi, lakini imejikita katika kutoa uthibitisho kwamba kwa kawaida hatujihusianishi na umasihi wake wa kweli, yaani matendo yake ya ukombozi, uponyaji, na kuwekwa huru miongoni mwa maskini, ambayo yanahusiana na yanapaswa kuhusianishwa moja kwa moja na kuwahubiria Injili ya Ufalme. Kwa mambo haya, twajua ya kuwa Yesu wa Nazareti ndiye Yule, Masihi wa kweli wa Mungu aliyekuja duniani.

Made with FlippingBook - Online catalogs