Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
4 6 0 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Wanafunzi hawataweza kusoma kwa hakika nukuu zinazotokea katikati ya somo wanapotazama video. Nukuu hizi, hata hivyo, zinaendana moja kwa moja na mada zinazofundishwa katika video, na mnaweza na mnapaswa kuziangalia na kuzijadili wakati wa vipindi vya marudio ya somo. Wakumbushe wanafunzi wako kwamba wakifundisha masomo haya kwa wengine, nukuu hizi zinaweza kuwasaidia sana katika kujitayarisha na kufundisha. Soma nukuu ya R. E. Nixon hapa chini na ujadili pamoja na wanafunzi wako muhtasari wake wa hali ya juu wa umaskini katika Agano Jipya. Wasaidie wanafunzi kuelewa jinsi hadhi ya maskini ilivyokuwa ya msingi kwa ujumbe halisi wa Ufalme wa Mungu. Waonyeshe kwa nini hadhi ya watu maskini lazima ichukuliwe kuwa jambo kuu na kipimo cha Ukristo wa aina yoyote unaodai kuongozwa na tumaini la Kimasihi la Agano la Kale, na asili ya Injili ya Ufalme Agano Jipya. Hongera! Umemaliza kikamilifu masomo yote ya darasani kwa moduli hii! Ingawa umekamilisha mafundisho ya darasani, kazi yako kama mwalimu na mkaguzi wa kazi sasa ndiyo inaanza rasmi. Ili wanafunzi waweze kukamilisha masomo yao, wanapaswa kukamilisha kazi zote zinazohusiana na kozi hii, zikiwemo kazi yao ya huduma kwa vitendo, kazi ya ufafanuzi wa maandiko (eksejesia), pamoja na kazi nyingine ulizowapa wakati wa kozi hii. Uwezo wako wa kupima matokeo na kutoa alama ya jumla kwa kila mwanafunzi bila shaka unategemea wao kuwasilisha kazi zao kwako, na wewe kuzifanyia tathmini kwa kuzingatia vigezo na viwango vilivyowekwa. Kuhusu kazi zinazowasilishwa kwa kuchelewa, utahitaji kutumia hekima na busara. Kama hutoweka muda maalum ambao wanafunzi wanapaswa kuwasilisha kazi zao kwako, wataendelea kuchelewesha kazi hizo bila kikomo. Lakini pia, ukiwa mkali kupita kiasi, unaweza kupuuza sababu halali ambazo wanafunzi wanaweza kuwa nazo. Ni muhimu kufanya uamuzi fulani kuhusu kazi zitakazo cheleweshwa; ukichagua kupunguza alama, huenda ikasababisha mabadiliko ya daraja la ufaulu. Unaweza pia kuchagua kuwapa baadhi ya wanafunzi daraja la “Kutokamilisha kazi” hadi kazi zao zitakapokamilika. Hata hivyo, bila kujali kanuni utakayoiweka kuhusu kazi zao, kumbuka kuwa kozi zetu si kwa ajili ya kupata alama pekee,
3 Ukurasa 188 Nukuu ya Kvalbein
4 Ukurasa 215 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
5 Ukurasa 227 Kazi
Made with FlippingBook - Online catalogs