Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

102 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

• Kuonyesha, kupitia matumizi binafsi ya Mbinu ya Hatua Tatu , namna ambavyo kila hatua moja ya hatua hizi muhimu inachambua kwa kina andiko minajili ya kubaini kwa uhakika kusudi la mafunuo yaliyomo ndani ya maana ya kifungu husika, na lile badiliko la maisha yetu litokanalo na furaha ya kugundua kanuni za kibiblia kwa ajili ya maisha. • Kutambua vipengele, tahadhari, na taratibu muhimu katika kuchunguza mazingira ya asilia ya andiko, kugundua kanuni za kibiblia, na kuhusianisha kwa usahihi fundisho la andiko katika maisha yako. Moyo Ulioandaliwa Kujifunza, Kutenda na Kufundisha Neno la Mungu. Ezra 7:10 – Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya Bwana, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli. Je, moyo wako umeandaliwa mbele za Mungu? Tunapowatazama watakatifu wakuu katika maandiko tunagundua kwamba Mungu wetu huwatumia wanaume na wanawake ambao mioyo yao imeandaliwa mbele zake kwa ajili ya kujifunza Neno lake, kulitendea kazi kwa bidii maishani mwao, ili hatimaye awatumie kama vyombo vyake kwa kusudi la kuwafundisha wengine kweli ya Neno lake. Labda moja ya mifano ya wazi zaidi kuhusiana na hili ni ule uliorekodiwa katika kitabu cha kihistoria cha Ezra katika Agano la Kale, ambacho kinaelezea kurudi kwa wana wa Israeli baada ya kipindi cha uhamisho, waliporudi Yuda kutoka BHabili kwa lengo la kuleta uamsho wa kiroho kwa waaminifu na kuanzisha upya ibada ya Bwana katika hekalu. Mada ya kumfanyia Bwana Ibada kwa njia inayofaa na sahihi ndio mada kuu katika vitabu vyote vya Agano la Kale vilivyoandikwa baada ya Israeli na Yuda kupelekwa utumwani kwa sababu ya dhambi waliyomtenda Mungu. Vitabu hivi ni 1 na 2 Mambo ya Nyakati, Ezra, Nehemia, Hagai, Zekaria, na Malaki (isipokuwa kitabu cha Esta). Wale waliorudi walikuwa tayari kukiri dhambi zao mbele za Bwana, wakiamini kwamba angewaweka tena katika nchi ambayo alikuwa amewapa, na kwamba Yeye peke yake ndiye aliyestahili kuabudiwa na ndiye ambaye angeweza kuuleta utawala wa ufalme wake katikati ya watu wake kupitia Masihi ajaye. Kimsingi kulikuwa na awamu tatu za kurudi kwa Wayahudi katika nchi ya Israeli kutoka BHabili, ambako kulitokea takriban miaka ya 538, 458, na 444 K.W.K. Hilo linaendana na ukweli kwamba walihamishwa pia kwa awamu tatu kutoka katika nchi ya Israeli kwenda BHabili miaka ya 605, 597, na 586 K.W.K. Awamu hizo za kurudi kwao ziliongozwa na watumishi waliomcha Mungu, awamu ya kwanza ikiongozwa na ZerubHabili mwaka wa 538 K.W.K. (Ezra

Ibada Ukurasa wa 77  2

2

M A S O M O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker