Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 2 | KUTAF S I R I B I B L I A : MB I NU YA HATUA TATU / 103
1-6; Hagai; Zekaria), ambaye jitihada zake zilisababisha kujengwa upya kwa hekalu. Kurudi kwa awamu ya pili kulitokea mwaka wa 458 K.W.K. chini ya uongozi na usimamizi wa Ezra (Ezra 7-10), ambapo mkazo mkubwa ulikuwa ni matengenezo ya watu na maelekezo, uamsho wao wa kiroho, na haja ya wao kurudi kwa Bwana kwa kulishika agano. Hatimaye, Nehemia aliongoza kundi la tatu la Wayahudi kurudi katika nchi mwaka wa 444 K.W.K., akiwa na mzigo mkubwa moyoni mwake wa kujenga upya kuta za Yerusalemu zilizokuwa zimebomolewa na, kwa kuungana pamoja na Ezra, kuwarudisha watu wa Mungu kwa Bwana wakiwa na hali mpya ya kiroho na kurejea katika utii wa agano. Wanazuoni wengi wanaamini kwamba huenda kitabu cha Malaki kiliandikwa katika nyakati za Nehemia, na kwamba kitabu cha Esta kiliandikwa wakati wa matukio yaliyorekodiwa katika Ezra sura ya 6 na ya 7. Kipindi hiki chenye matukio mengi katika historia ya Israeli kinatusaidia kupata ufahamu muhimu unaohitajika kwa ajili ya kuwaandaa wanaume na wanawake wenye wito wa kazi ya Mungu. Andiko letu moja la kipengele hiki cha ibada limerekodi aina ya maisha ya ndani na nia ya mtu ambaye Mungu anamtumia kuleta uamsho, upya, na burudiko kwa watu wake. “ Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya Bwana, na kuitenda, na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli .” Kulingana na andiko letu, Ezra alikuwa “ameuelekeza moyo wake,” kwa maana halisi “ameikaza nafsi yake” kufanya mambo matatu kwa ajili ya Bwana. Kwanza, Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kusoma Sheria ya Bwana. Huu si ule usomaji nusu-nusu wa Neno la Mungu, wa macho yenye usingizi, bali ni kujifunza Sheria ya Mungu kwa nidhamu, shauku, na umakini mkubwa. Biblia haiwezi kueleweka kwa njia nyingine; pasipo kutafuta maarifa ya Bwana kama wawindaji wa hazina wanavyotafuta dhahabu, hatuwezi kugundua wala kuelewa kina kilichofichwa ndani ya andiko na maana yake (Mit. 2:1-9). Moyo mvivu, usio na nidhamu kamwe hautakuja kujua utajiri wa hekima ya Mungu kuhusu mpango wake wa wokovu katika Kristo. Pili, alikuwa ameuelekeza moyo wake kwa dhati kulitendea kazi Neno. Kwa ufupi, Ezra hakuishi ili kujifunza, badala yake, alijifunza ili kuishi. Kusudi la Neno la Mungu sio tu kusikia mapenzi ya Mungu kuhusu imani, utii, upendo, na huduma. Kusudi ni kulitendea kazi, na mbaraka uliomo katika andiko hauhusiani kabisa na wale wanaolitafakari tu bali kwa wale wanaoliitikia, yaani kuliishi kwa unyenyekevu na bidii kwani ni Neno la Mungu (Yakobo 1:22 25). Hekima ya Bwana huwajia wale wanaofanya mapenzi yake kwa dhati wanapoyagundua katika Neno lake takatifu (rej. Zaburi 111:10 - Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele!).
2
M A S O M O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker