Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

104 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Mwisho, Ezra aliuelekeza moyo wake “ kufundisha maagizo na hukumu zake katika Israeli .” Mtumishi wa Mungu akiweza kulimudu Neno la Mungu kwa kujifunza na kuliishi kwa tii, basi atakuwa tayari kutimiza huduma yake kupitia huduma ya kufundisha. Vipaumbele vya Ezra kuhusu namna ya kuiendea huduma yake ya Neno vilikuwa katika mpangilio makini: alijiandaa kujifunza Sheria ya Mungu kamilifu, kuitendea kazi, na kisha kuifundisha. Aina hii ya kujiwekea nidhamu kwa umakini na kuwa na maandalizi ya moyo ni sifa muhimu ambayo watakatifu, watenda kazi wa Kikristo, manabii, na mitume wanayo. Mkazo wao si juu ya umisheni, au kazi, au baraka, au karama. Mkazo wao ni juu ya Neno la Mungu— kulisoma, kulifahamu, kuliweka katika vitendo, na kisha, baada ya kulijua na kulitii, inafuata hatua ya kulifundisha kwa shauku na uwazi. Hiki ndicho hasa kilichotokea katika huduma ya Ezra kwa watu; kwa sababu ya vipaumbele vya moyo wake, Mungu alimtumia kwa nguvu kuleta uamsho na upya kwa watu wa Mungu, na kuweka msingi wa harakati ambayo hatimaye ingeliandaa taifa kwa ajili ya ujio wa Masihi. Na haya yote, kwa sababu mtu mmoja tu aliyempenda sana Mungu aliuandaa moyo wake kwa ajili ya kulifanyia nafasi Neno la Mungu. Moyo wako umeandaliwa mbele za Mungu ili kujifunza, kutendea kazi, na kufundisha Neno lake kwa watu wake na kwa utukufu wake? Kipaumbele chako ni nini – vipawa vyako, baraka zako, fursa zako, au unayo shauku ya kweli ya kulifahamu Neno la Mungu ili uweze kuliweka katika vitendo maishani mwako, na kuwa tayari kuongozwa na Roho Mtakatifu kufundisha Neno la Mungu kwa watu wake? Hebu tujifunze kupitia mfano wa mhubiri huyu mnyenyekevu na jasiri wa Neno la Mungu ambaye huduma yake haikuanza na mikakati mikubwa ya kutafuta nguvu ya ushawishi, bali kwa unyenyekevu na kuuelekeza moyo wake kuyajua na kuyafanya mapenzi ya Mungu kama alivyojifunza katika Neno la Mungu. Hiki ndicho kielelezo cha kweli cha huduma yoyote yenye matunda kwa ajili ya utukufu wa Jina la Bwana.

2

M A S O M O Y A B I B L I A

Baada ya kutamka na/au kuimba ukiri huu wa imani (taz. Kiambatisho) omba maombi yafuatayo:

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

Ee Mungu Mwenyezi, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo: Tunaomba utujalie kuwa na msingi na uthabiti katika Kweli yako kupitia ujio wa Roho Mtakatifu ndani ya mioyo yetu. Tusiyoyajua yafunue; yale yanayopungua ndani yetu, uyajaze; yale tunayoyajua, yathibitishe; na utulinde mbali na hatia katika utumishi wako; kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Amina.

~ Presbyterian Church (U.S.A.) and Cumberland Presbyterian Church. The Theology and Worship Ministry Unit. Book of Common Worship . Louisville: Westminister/John Knox Press, 1993. uk 26.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker