Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 2 | KUTAF S I R I B I B L I A : MB I NU YA HATUA TATU / 105

Pitia pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu andiko la kukumbuka la kipindi kilichopita, yaani 2 Timotheo 3:16-17.

Mazoezi ya Kukariri Maandiko

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za Kukusanya

KUJENGA DARAJA

Ni Mafunzo Rasmi Pekee ndio Yanayofaa Makanisa na madhehebu mengi siku hizi yanaamini kwamba wale wanaotamani kuingia katika huduma lazima wawe wamepitia mafunzo rasmi katika Chuo cha Biblia, Chuo cha Sanaa ya Kiliberali ya Kikristo, au Seminari. Wale walio na maoni kama hayo wanaamini kwamba maandalizi yasiyo rasmi ya mtu binafsi hayatoshi kumwezesha kukabiliana na ugumu, matatizo na changamoto za huduma. Badala yake, wanaamini kwamba mafunzo rasmi yanaweza kuongeza uwezekano wa mtu kufanikiwa katika utumishi na huduma yake. Kwa bahati mbaya, kwa wale wasio na uwezo wa kumudu gharama za mafunzo kama hayo au ambao hawana sifa za kujiunga na mifumo rasmi ya mafunzo, kwa mtazamo huu, moja kwa moja wamenyimwa nafasi na fursa na kuingia katika huduma. Nini maoni yako kuhusu nafasi ya mafunzo rasmi ya Biblia, theolojia, na ya kichungaji katika suala la huduma katika maeneo ya mijini? Je, inawezekana kuwa na huduma yenye matokeo mijini pasipo kupitia mafunzo rasmi ya huduma na utumishi? Ikiwa hilo linawezekana, maandalizi rasmi ya kitaaluma yana nafasi gani katika suala la huduma mijini? Kutambua Nia ya Roho Mtakatifu ndio Njia Yangu Ingawa wengi wanaamini kwamba kuwa na mbinu iliyo wazi na yenye mantiki ya kujifunza Biblia ni muhimu ili kutambua maana ya maandiko, wengi sana leo wanaendelea kuwa na mashaka kuhusu umuhimu wa mbinu katika kutambua mambo ya rohoni. Kwa sababu ya mashaka na mkanganyiko unaosababishwa na uhakiki wa kisasa wa historia ya Biblia, wengi wanaamini kwamba kukumbatia kwa namna yoyote mbinu fulani ya kujinza Biblia ni jambo hatari sana. Badala ya kutumia mbinu za kitaalamu kujifunza kweli za Neno, wao mara nyingi husisitiza zaidi matumizi ya njia na mitazamo ya kiroho katika kujifunza Biblia. Wanachukulia kujifunza Biblia kama mchakato wa kiroho sio wa kiakili, na wanataka kufundishwa na

1

2

M A S O M O Y A B I B L I A

2

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker