Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

106 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

Roho Mtakatifu. Hawachukulii kujifunza kama jambo linalohitaji kufuata mfumo au mbinu fulani, bali ni maandalizi ya moyo na nafsi ambayo humruhusu Roho Mtakatifu mwenyewe kuwa mwalimu wao. Wanahoji Ikiwa, kimsingi, Roho Mtakatifu pekee ndiye mwalimu wa kweli wa Neno la Mungu, kuna manufaa gani ya kutafuta mbinu ya kusoma, kujifunza, na kutumia maandiko? Ni kwa njia gani kuzingatia kwa umakini mbinu za kutafsiri Biblia kunaweza kusaidia au kuzuia uelewa wetu wa Neno la Mungu?

Mtazamo au Mbinu: Kipi ni Muhimu Zaidi katika Kutafsiri Biblia?

Ingawa wengi hukiri kwamba mbinu fulani ya kujifunza maandiko kwa nidhamu husaidia kuelewa kusudi la Mungu na maana ya kile anachozungumza katika Biblia, mara nyingi haieleweki wazi jinsi ya kupima umuhimu kati ya mtazamo na mbinu katika kujifunza. Kwa upande mmoja, wengi wanaamini kwamba pasipo kuwa na mtazamo mzuri, haiwezekani kuyaelewa maandiko. Haijalishi mbinu tunayoweza kuitumia kuelewa maana ya Biblia, inahitajika roho ya unyenyekevu na moyo uliovunjika na kupondeka ambao Mungu anasema katika maandiko kuwa ni dhabihu ya kweli mbele zake na kigezo cha uongozi wa kimungu na mafundisho ya Neno lake. Kwa upande mwingine, tunaweza kutaja mifano mingi ambapo unyenyekevu na fadhili, bidii na shauku pasipo maarifa vilileta matokeo ya kutisha ya kiroho. Mtazamo mzuri bila ujuzi hauwezi kuzaa ufahamu wa kiroho bali huzaa udhalimu, mkanganyiko, hata uzushi. Kuna uhusiano gani kati ya maandalizi sahihi ya moyo na mtazamo, na kufuata njia na mbinu yenye nidhamu ya kujifunza Biblia? Tunawezaje kuyaweka haya katika uwiano mzuri tunapojifunza maandiko?

3

2

M A S O M O Y A B I B L I A

Mbinu ya Hatua Tatu Kuziba Pengo kati ya Ulimwengu wa Kale na wa Sasa

Mch. Dr. Don L. Davis

MAUDHUI

Mbinu ya Hatua Tatu ni mbinu fasaha ya kutafsiri Biblia iliyotengenezwa ili kutusaidia kuelewa kweli za maandiko na kuziba pengo kati ya ulimwengu wa kale na wa sasa. Inalenga zaidi juhudi zetu za kutaka kuielewa hadhira ya kwanza ya andiko, kugundua kanuni za jumla za Neno, na kuzihusianisha na maisha ya kila siku.

Muhtasari

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker