Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

112 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

5. Tuna uwezekano mkubwa wa kufanya makosa ya kijiografia, kihistoria na kijamii .

B. Kwa nini ni vigumu sana kuelewa mazingira ya kihistoria ya andiko?

1. Hatukuwepo!: hakuna mtu aliye hai leo aliyekuwepo wakati wa matukio yanayoripotiwa katika maandiko.

2. Hatufahamu kwa ufasaha matumizi au tofauti za lugha za Biblia (Kiyunani, Kiaramu, na Kiebrania).

3. Mifumo yetu binafsi ya kupokea na kuchuja maoni mara kwa mara inazuia uelewa wetu wa mazingira ya kihistoria ya maandiko.

2

M A S O M O Y A B I B L I A

4. Tumezoezwa kusoma maandiko kama tunavyoyasoma siku zote (yaani, tunaingiza tafsiri za usomaji wa zamani katika usomaji wetu wa sasa).

5. Tunaharakisha kutoa hitimisho bila kuzingatia andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji au wasikilizaji wa kwanza.

C. Mtazamo muhimu unaohitajika: unyenyekevu , Yakobo 1:5

1. Kutambua muda mrefu unaotutenganisha na muktadha halisi wa andiko.

2. Utayari wa kukiri tofauti na vizuizi vilivyopo kati ya wakati wetu na ule wa waandishi na hadhira ya maandiko.

3. Utayari wa kuahirisha hitimisho hadi tutakapojifunza zaidi kuhusu muktadha asilia kabla ya kuhitimisha juu ya kile ambacho andiko lilimaanisha lilipoandikwa.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker