Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 2 | KUTAF S I R I B I B L I A : MB I NU YA HATUA TATU / 121

Mungu kwetu kupitia nafsi na kazi ya Yesu Kristo? Tolea mifano jibu lako. 5. Eleza kwa ufupi mbinu ya sarufi ya kihistoria ya kujifunza Biblia na namna inavyohusiana na Mbinu ya cha Hatua Tatu. Kwa namna hiyo, ni jinsi gani Mbinu ya Hatua Tatu inatusaidia kuelewa maana iliyo wazi ya kifungu, na muunganiko wa ujumbe mzima wa Biblia? 6. Kwa nini ni muhimu kuheshimu umoja wa maandiko kama yalivyotujia katika aina zake mbalimbali (k.m., mashairi, nyimbo, nyaraka, historia, n.k.), na ni jinsi gani Mbinu ya Hatua Tatu hutusaidia kufanya hivyo? 7. Eleza kwa ufupi sababu muhimu zinazohusika katika kila hatua ya Mbinu ya Hatua Tatu. Ni kwa jinsi gani kila moja ya hatua hizo tatu inatusaidia kushinda baadhi ya matatizo yanayohusiana na kuelewa kile ambacho Biblia inafundisha kama maandiko ya kale yaliyoandikwa katika lugha ambazo hazizungumzwi tena au kutumiwa kama zilivyokuwa wakati wa kuandikwa kwa Biblia? Elezea jibu lako vizuri. 8. Unyenyekevu, umakini, na kupenda uhuru katika Kristo huathirije uwezo wetu wa kulifahamu na kulitumia Neno la Mungu? Kuna uhusiano gani kati ya mtazamo na mbinu katika kutafuta kutambua maana ya Biblia? Kipi ni muhimu zaidi kati ya mtazamo na mbinu? Toa mfano ili kufafanua maoni yako. 9. Elezea na utetee kauli hii: “namna yoyote halali ya kutafsiri Biblia lazima ilenge kulifahamu Neno la Mungu kwa dhumuni la kuleta badiliko katika maisha, na si habari ya kujaza taarifa akilini.” Je, Mbinu ya Hatua Tatu inasaidiaje

2

M A S O M O Y A B I B L I A

kuweka mkazo wetu katika badiliko la maisha na sio uchanganuzi wa maandiko na misamiati peke yake?

UHUSIANISHAJI

Kufikia ustadi na umahiri katika Neno la Mungu ni jambo la msingi na hitaji muhimu sana kwa kila mwanamume na mwanamke mtumishi wa Mungu, kwa sababu ni maandiko yenye pumzi ya Mungu pekee yanayoweza kutufanya watenda kazi hodari na watumishi waaminifu wa Kanisa, ili kutuwezesha kuwaandaa wengine kwa ajili ya huduma, na kuhudumia mahitaji halisi ya wale walio ndani na nje ya Kanisa (2 Tim. 3:16-17). Hakuna namna bora tunayoweza kukazia sana umuhimu wa uwezo wako wa kulitumia Neno kwa usahihi ( 2 Tim. 2:15 ), kutafakari juu Neno mchana na usiku ili uweze kufanikiwa katika yote utendayo kwa ajili ya Mungu ( Yos. 1:8 ), na kuwa na uhakika juu ya aina ya matokeo na nguvu

Muhtasari wa Dhana Muhimu

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker