Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
122 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
unayotamani katika kila hatua ya utumishi wako kwa Bwana (Zab. 1:1-3). Zifuatazo hapa chini ni dhana kuu ambazo tumejifunza katika somo hili la Mbinu ya Hatua Tatu , kwa hivyo tafadhali zipitie kwa bidii na kwa umakini. Kuelewa mbinu hii kunaweza kukuwezesha kupata ujuzi na ustadi wa kuwa mtenda kazi wa maandiko, mwenye kukubaliwa na Mungu na usiye na sababu ya kutahayari unapotulimia Neno lake kwa usahihi na uhalali. • Mbinu ya Hatua Tatu ni mbinu fasaha ya kutafsiri Biblia iliyotengenezwa ili kutusaidia kuelewa kweli ya maandiko na kuziba pengo lililopo kati ya ulimwengu wa kale na wa sasa. Mbinu ya Hatua Tatu inafafanuliwa kama “kuelewa maana iliyokusudiwa katika mazingira ya kwanza ya andiko ili tuweze kugundua kanuni za jumla za Kweli ya Neno ambazo zinaweza kutumika katika maisha yetu binafsi ndani ya uhuru wa Roho Mtakatifu.” • Ingawa kusoma maneno mahususi, vifungu vya maneno, aya, sura, sehemu, na vitabu vya Biblia ni jambo la kujenga na la lazima, ufahamu wetu wote katika maandiko unapaswa kuendana na ujumbe wa Biblia nzima, yaani, maana na ujumbe wa ufunuo wa mwisho wa Mungu kwetu katika nafsi na kazi ya Yesu Kristo. • Mbinu ya Hatua Tatu inaakisi na kuendana na mbinu ya sarufi ya kihistoria ya kutafsiri maandiko, ambayo inahakiki na kuthibitisha maana ya wazi ya maandiko katika Biblia, ufunuo endelevu wa Mungu kwa njia ya Kristo, umoja wa Biblia, na usahihi wa andiko katika kuwasilisha ujumbe kwetu kwa kutumia tanzu na miundo tofauti ya fasihi. • Kila hatua inayohusika katika Mbinu ya Hatua Tatu ina lengo na mantiki yake mahususi, kadhalika ina sababu na msingi, na mitazamo muhimu, na inatimizwa kwa fuata mpangilio na orodha maalum ya vipengele. Ili kuweza kutumia mbinu hii lazima tuwe na ufahamu na ujuzi kuhusiana na hatua husika na vipengele vyake. • Katika kujiandaa kutumia njia yoyote ya kujifunza Biblia, jambo kubwa na la msingi zaidi ni mtazamo wa mwanafunzi wa maandiko, kwa sababu hatua hizi za kujifunza kupitia Mbinu ya Hatua Tatu zinadai unyenyekevu, bidii, na uhuru katika kila hatua. • Kama watumwa wa haki chini ya ubwana wa Kristo, tumeitwa kulitii Neno lake katika kila nyanja ya maisha na huduma zetu, kwa hiyo, namna yoyote halali ya kutafsiri Biblia lazima ilenge katika kulifahamu Neno la Mungu kwa madhumuni ya kuleta badiliko katika maisha , na si habari ya kujaza taarifa akilini .
Umuhimu wa Msomaji wa Kwanza: Ufunguo wa Mbinu ya Hatua Tatu
Wafasiri na wakalimani
wanapojiuliza ni kwa namna gani
wasomaji wa kwanza wangeelewa kifungu fulani, hawaulizi swali la kidhahania tu ambalo haliwezekani kujibu (kwa kuwa hatuna uwezo wa kuingia katika akili na fikra zao). Badala yake, hii ni njia rahisi ya kutupeleka kwenye maswali mengine madogo: Je! Maneno haya yangeelewekaje wakati huo? Ni maswala na mada gani zilikuwa za umuhimu mkubwa? Andiko hili la Biblia lingeweza kukabiliana na aina haya hakumaanishi kwamba tunaweza kupata majibu kamili wakati wote. Wakati mwingine tunaweza kukisia majibu sahihi kwa kuyalinganisha maandiko yenyewe. ~ Donald A. Carson. New Bible Commentary: 21st Century Edition. (nakala ya kielektroniki la toleo la 4). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1997. gani ya mfumo wa fikra? Kuuliza maswali kama
2
M A S O M O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker