Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
128 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
na ndiye pekee anayetosha kutufundisha maana na umuhimu wa maandiko katika maisha yetu leo. Kumtegemea Roho Mtakatifu kunakuza na kuzidisha bidii yetu ya kusoma na kujifunza Neno , hata hivyo hakujakusudiwa kuwa mbadala wa juhudu na bidii hiyo ya kujifunza Biblia. Hatua za Mbinu ya Hatua Tatu ni rahisi na za wazi. Kwanza, tunachunguza yaliyomo katika andiko, tukiangazia historia ya kitabu husika, mwandishi wake na hadhira yake (wasikilizaji au wasomaji wake), madhumuni ya kuandikwa kwake, pamoja na namna kilivyotasfiriwa katika tafsiri mbalimbali. Kisha, tunagundua kanuni za jumla ambazo zinatoa muhtasari wa maarifa tuliyoyapata kuhusiana na maana ya andiko husika katika muktadha wake wa awali , na maana ya andiko hilo kwetu, katika maisha yetu leo . Hatimaye, tunatumia kanuni hizo za kiroho katika maisha yetu kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Tunapoonyesha utiifu wa mioyo yetu kwa Mungu, tunapaswa kukumbuka mafundisho ya kawaida yanayosisitizwa katika maandiko yote ambayo ni msingi wa mapenzi yake kwa waamini wote katika Agano la Kale na Agano Jipya— kumpenda Mungu na kumpenda jirani kwa njia ya imani katika Kristo, yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Kama unapenda kujifunza kwa kina baadhi ya mawazo yaliyomo katika somo hili la Kutafsiri Biblia: Mbinu ya Hatua Tatu , jaribu kusoma vitabu hivi: Fee, Gordon D. New Testament Exegesis: A Handbook for Students and Pastors . Toleo la 3. Louisville, KY: Westminster John Knox Press, 2002. Grenz, Stanley J., na Roger E. Olson. Who Needs Theology?: An Invitation to The Study of God . Downers Grove, IL: Intervarsity, 1996. Grenz, Stanley J., na John R. Franke. Beyond Foundationalism: Shaping Theology In a Postmodern Context . Louisville, KY: Westminster John Knox Press, 2000. Stuart, Douglas K. Old Testament Exegesis: A Handbook for Students and Pastors . Toleo la 3. Louisville, KY: Westminster John Knox Press, 2001. Traina, Robert A. Methodical Bible Study . Grand Rapids: Zondervan Publishing Company, 1985. Huduma yoyote halali ya Ufalme ina msingi wake katika kutendea kazi Neno lenye pumzi ya Mungu, yaani maandiko. Kama tulivyoona kwa Ezra katika kipengele chetu cha ibada, uwezo wako wa kusoma Sheria ya Bwana na kuitenda ndio ufunguo wa kukuwezesha kufundisha Kweli ya Mungu katikati ya watu wake, Kanisa, na kwa
2
Nyenzo na Bibliografia
M A S O M O Y A B I B L I A
Kuhusianisha Somo na Huduma
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker